Changamoto Yatolewa Uhifadhi wa Uoto wa Mistu ya Miombo

Washiriki wa mafunzo ambao ni waratibu wa mradi wa miombo kutoka Wilaya za  mikoa ya Tabora na Katavi wakimsikiliza Katibu Tawala

Washiriki wa mafunzo ambao ni waratibu wa mradi wa miombo kutoka Wilaya za mikoa ya Tabora na Katavi wakimsikiliza Katibu Tawala

Na Kibada Ernest –Kibada.

Changamoto Imetolewa kuwa uhifadhi wa misitu ya asili ya uoto wa miombo ni muhimu kuihifadhi na kuitunza kwa Mstakabali wa maisha ya kizazi kijacho na iwapo itatoweka katika sura ya uso wa dunia ardhi itageuka jangwa hivyo kuleta umasikini kwa jamii.
Changamoto hiyo imetolwa na Katibu Tawala Msaidizi Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi Bw,Salum Shilingi wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa maafisa wa kilimo na mistu wanoshughulikia mradi wa miombo katika Mikoa ya Katavi na Tabora.
Mafunzo hayo ni kwa ajili ya matumizi ya vifaa vya elektroniki vitakavyotumika kukusanyia takwimu za kuhifadhia kumbumbuku za mradi wa miombo iikiwa ni pamoja na upigaji picha za mnato na video,GPS na Simu za mkononi za smartphone kwa ajili ya kutumia taarifa mbalimbali ya maendeleo ya mradi kama kuna uharibifu umejitokeza au hali halisi ya maendeelo ya mradi.

Mratibu wa miyombo kwa Mikoa ya Tabora na Katavi Yuob Kiumbe akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wa miombo kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala Msaidizi kufungua Mafunzo ya waratibu wa Waratibu wa wilaya wa mradi.

Mratibu wa miyombo kwa Mikoa ya Tabora na Katavi Yuob Kiumbe akitoa maelezo mafupi kuhusu mradi wa miombo kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala Msaidizi kufungua Mafunzo ya waratibu wa Waratibu wa wilaya wa mradi.


Mafunzo hayo kwa watalaam yatasaidia kuboresha utendaji wa kazi na taarifa zitakazokuwa zikiandaliwa zitakuwa na ubora kwani zitakuwa zimeboreshwa zaidi na zitambata na picha kuonesha uhalisia wa hali ilivyo ama ya maendeleo ya uhifadhi wa misitu ya miombo.
Yanawahusisha watalaam kutoka Idara ya Mistu na nyuki,pamoja na Idara ya Kilimo kutoka Mkoa wa Katavi na Tabora ambayo wilaya zake zinatakeleza mradi wa miombo.
Shilingi akizungumzia kuhusu ufadhili wa mradi ambao ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP ambao ndio ndio wanafadhili Mradi pia wametoa vifaa ambavyo ni vitendea kazi ambavyo ni GPS,Simu za Mkononi aina ya Huwaei Kisasa,zinazoweza kutumika kutuma taarifa,Camera za picha za Mnato na Picha Video vitakavyotumiwa na watalaam wanaosimamia mradi huo.
.
Kwenye Program ya miombo ipo miradi mbalmbali itakayokuwa ikitekelezwa katika maeneo ya wilaya husika kama ufugaji nyuki,ufugaji samaki, kilimo pamoja na nyingine zitakazowawezesha kujipatia kipato bila kuathiri uharibifu wa mistu na uoto wa asili wa miombo.a na kuwaondolea umasikini.
Lengo la mradi wa miombo ni kuwasaidia jamii kuondokana na umasikini,kuiondoa jamii katika umasikini kutokana na rasilimali ya mistu ya miombo iliyoko kwenye eneo husika jamii kwa kuijengea mazingira yatakayowafanya wajishughulishe na shughuli uzalishaji mali ambazo haziathiri mazingira.
Aidha amesisitiza mafunzo yaliyopatikana yasaidie kuboresha utendaji kazi na vifaa vya kisasa visaidie kurahisisha ukusanyaji wa takwimu na kuweka kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kuboresha mradi.
Akasisitiza watendaji hao kuwasaidia wanajamii kuondokana na umasikini kwa kuwa wanajamii wanao utajiri wa miti ya miombo,kama ilivyo kauli mbiu ya miombo,isemavyo “miombo utajiri” “utajiri miombo”.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa miombo kwa mikoa ya Tabora na Katavi Youb Kiungo alieleza kuwa mradi wa miombo unatekelezwa katika wilaya nne zilizoko mkoani Tabora na wilaya moja iliyoko mkoani Katavi.
Kiungo alizitaja wilaya hizo kuwa Sikonge,Urambo,Kaliua na Sikonge zilizoko Mkoani Tabaora na Wilaya moja ya Mlele iliyoko Mkoa wa Katavi ambapo wilaya hizo zina mistu ya uoto wa miombo.na sehemu kubwa ya misitu hiyo ikiwa upande wa mkoa wa Katavi.
Mratibu huyo alieleza kuwa mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na ulianza kutekelezwa mwaka 2013 lakini umeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa jamii imeanza kuelewa umuhimu wa kuhifadhi na kutunza uoto wa mistu ya miombo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo kutoka wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora Evan Mvurungu amabaye ni Afisa kilimo na Ushirika alieleza kufurahishwa na mafunzo waliyoyapata ya utumiaji wa vifaa vya kiektroniki kwa ajili ya shughuli za mradi wanategemea kuwa taarifa zao zitakuwa zikitayarishwa kwa ustadi mkubwa.

Mvurungu ameeleza kuwa Vifaa vya kufanyia kazi walivyopatiwa vitasaidia kuongeza ari yakazi na hawaoni sababu ya kutokutekeleza shughuli kwa ubora bila kuweka viisingizio vya kutekeleza kazi zao kwa ufasaha.