Tanzania Kupambana na Ukosefu wa Lishe bora
LISHE BORA ni msingi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Saada Salum Mkuya alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano kuhusu suala la Lishe (Nutrition).
“Ni muhimu kuelewa madhara yatakayompata mtoto ikiwa mama hata mnyonyesha mtoto huyo ikiwa ni pamoja na athari mbaya juu ya mwili na maendeleo ya mtoto kutoka mimba mpaka kufikia umri wa miaka miwili kama mtoto hatapat Madhara haya ni kubatilishwa.,” Alisema Mkuya.
Mkuya aliongeza kuwa, “ Tanzania tunajitahidi sana kupambana na janga hili kwani mama kushindwa kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita kunaweza kusababisha utapiamlo na kusababisha kuathiri mamilioni ya watu katika Tanzania, hasa watoto, na hivyo kusababisha magonjwa kuenea na kunyong’onyesha maendeleo ya kimwili na ki akili”.
“Kwa kuruhusu hali hiyo kunachangia kupunguza uwezo katika kuboresha uwezo wakufikiri, kupunguza nguvu ya kujifunza na kuwa mbunifu, kuongezeka kwa umaskini, na kasi ndogo katika kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi”.Aliongeza Mkuya.
Takwimu za mwisho za utafiti wa mambo ya afya zina onyesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 5-59 wana upungufu wa madini,asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa vitamin A. Asilimia 11 ya wanawake wenye umri wa kuzaa yaani miaka 15-49 wana uzito wa chini, asilimia 41 wana uzito wa chini na upungufu wa madini, wakati asilimia 58 ya mama wajawazito wana upungufu wa madini pia.
“Katika Tanzania mikoa ambayo inafanya vizuri katika kupambana na utapiamlo ni mkoa wa Kilimanjaro, Mjini magharibi na Mkoa wa Dar es salaam.” Alisema Mshauri Lishe wa Rais Jakaya Kikwete”.Dr. Wilbald Lori.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na janga hili, hivyo katika mikutano hii mikakati mbalimbali inapangwa ya jinsi ya kulimaliza kabisa tatizo hili.
Mikutano hii bado inaendelea na hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi.