Na Mwandishi Wetu, Tanga
MASHINDANO ya mbio za Magari ya “Zig Zag Tanga Rally 2015” yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi mkoani Tanga Mei 3 mwaka huu mzunguko wa pili kwenye yale ya Kitaifa chini ya ufadhili wa Zig Zag.
Mashindano hayo watashindanisha umbali wa km 135 na yatakuwa na awamu tano, yatakayoanzia katika hotel ya Tanga Beach Resort na kupitia maeneo ya Pongwe, Mkanyageni na Mjesani na kurudi yalipoanzia.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Mehul Asher alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri ambapo washiriki kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini. Alisema kuwa madereva watakaoshiriki katika michuano hiyo wanatazamiwa kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga ikiwemo wengine kutoka nchi za Kenya na Uganda.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mashindano hayo msimu huu yatakuwa na upinzani mkubwa kutokana na barabara watakazotumia washiriki ni nzuri hivyo itaweze kuwapa fursa kushindana vema. Aidha alisema kuwa makabidhiano ya zawadi zilizoandaliwa kwa washindi mbalimbali zitafanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mara baada ya kumalizika mashindano hayo.
Hata hivyo alisema kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fennela Mukangara