Na Janeth Mushi, Arusha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, jana amemsomea mashitaka
13 ya uhujumu uchumi wa nchi kwa kughushi nyaraka na kujipatia fedha
zaidi ya sh. bilioni 18 Wakili maarufu jijini hapa, Medium Mwale
akiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ambako amelazwa
kwa matibabu.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles
Magesa mwendesha mashitaka wa Serikali, Fredrick Manyanda, alidai kuwa
kesi hiyo inayomkabili Wakili Mwale ya kudaiwa kujipatia bilioni 18 fedha alizojipatia kwa njia haramu.
Mwendesha mashitaka huyo alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo kwa kuhamisha fedha hizo kwa kampuni tofauti kwa siku tofauti,
ambazo alizitaja kuwa ni kampuni ya Olive Green, Nyamao Mbeche Hollo,
Gregg Motachwa, Ogembo Meetchel, John Adam na Mosoto Haye.
Manyanda alidai kuwa mshitakiwa alikuwa akihamisha fedha hizo kutoka
kampuni moja kwenda nyingine hadi kufikia kwenye akaunti yake na
kujipatia fedha hizo zaidi ya sh. bilioni 18.
Aidha mshitakiwa huyo alikana mashitaka hayo yote 13 baada ya
kusomewa akiwa wodini huku akiwa amezungukwa na Maofisa usalama wa
Taifa na maaskari, huku akiwa katika hospitali hiyo ya Mt. Meru kwa
muda wa wiki moja. Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo Agosti 31 mwaka huu itakapotajwa tena, katika Mahakama ya hakimu Mkazi mkoa wa Arusha.
Awali kesi hiyo ilishindwa kusomwa Mahakamani hapo Agosti 9 mwaka
huu baada ya upande wa utetezi kukataa mashtaka yanayomkabili Mwale
kwa madai kuwa majina ya kampuni hayakuandikwa kwenye hati ya
mashitaka.
Magesa alisema kuwa katika mashtaka 13, shitaka la 3-13 halioneshi
moja kwa moja kama Mwale amelipwa au amepata fedha kupitia kampuni
gani na pia haionyeshi kama fedha hizo ni za kampuni, taasisi au
shirika bali katika hati ya mashtaka, inadai fedha hizo zililipwa kwa
kupitia kampuni fulani ambayo haijatajwa jina wala kutolewa ufafanuzi
wake mahakamani hapo.
Wakili Upande wa Utetezi Loum Ojare alisema, hawayakubali mashtaka
yaliyoorodheshwa mahakamani hapo na upande wa Serikali, hivyo ni vyema
wakakaa na kuyarudia upya mashtaka hayo, ili mshtakiwa Mwale aweze
kujua anakabiliwa na mashtaka mangapi na yanahusiana na nini, kuliko
kumtuhumu kwa mashataka ambayo hayajajitosheleza.
Baada ya mgongano huo wa kisheria Hakimu, Magesa aliahirisha kesi kwa
muda na kutoa maamuzi ya kuwa upande wa Serikali uandae upya mashataka
yanayomkabili Mwale na kuhakikisha hati itakayofikishwa mahakamani
hapo, iwe sahihi na haina makosa kwania hati iliyoletwa hapo awali
haijajitosheleza na wala hainonyeshi ni kampuni gani inayohusika kumpa
fedha hizo pamoja na vitu vingine.
Baada ya Hakimu Magesa kuahirisha kesi hiyo upande wa mashtka hawakuwa
tayari kutoa hati ya mashtaka ambayo walikuwa wameiandaa hapo awali na
kutumika kumsomea mashtaka Mwale japo kuwa waliikosea.