Na Kibada Enest, Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Dk. Ibrahimu Msengi ameshauri Uongozi wa Chuo Kikuu Huria tawi la Mkoa wa Katavi kuwa wabunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato kuliko kutegemea Ada ya wanafunzi na ruzuku ya serikali katika kujiendesha kuliko kutegemea pato moja tu ambalo ni ada ya wanachuo.
Ametoa rai hiyo wakati akihutubia Jumuiya ya wananchuo na wananchi kwenye hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof, Tom Mbwete aliyemaliza muda wake kukiongoza chuo hicho na sasa anakwenda kuhudumia maeneo mengine katika nchi za Bara la Afrika.
Dk. Msengi amesema uongozi wa Chuo Kikuu Huria Mkoani humo utumia fursa zilizopo katika Mkoa kuhakikisha wanakuwa wabunifu kupata vyanzo vya mapato, ambapo wamepata eneo la kujenga Chuo akashauri waweke miundo mbinu itakayoasaidia kukiingizia chuo mapato kama kujenga kumbi kubwa zitakazotumika kwa ajili ya mikutano mbalimbali, pamoja na kumbi za semina kwa wanafunzi, na pengine watu kutoka nje wanaweza kuja kukodisha na kuweza kukiingizia Chuo mapato.
Awali Meneja wa Chuo hicho tawi la Katavi Newton Kyando ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo hicho alieleza kuwa chuo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo na ukata wa fedha, mwamko mdogo wa elimu miongoni mwa baadhi ya wananchi Mkoani humo katika kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu huria, pamoja na uchache wa watumishi katika tawi la Katavi.
Changamoto nyingine alieliza kuwa ni ukosefu wa maktaba pamoja na upungufu wa watumishi pamoja na uchache wa fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya uendeshaji ambapo fedha inayoletwa ni ndogo ambayo haitoshelezi uendeshaji wa ofisi.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria anayemaliza muda wake Prof. Tomu Mbete akitoa neno la shukurani kwa wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria tawi la Katavi aliwashukuru kwa juhudi zao za kukifanya chuo hicho kiweze kuwa na wanafunzi na wananchi mkoani humo wameonekeana kuwa na mwamko wa kukitumia kujipatia elimu.
Prof Mbwete akaeleza kuwa kwa sasa anaenda kutumikia wananchi wengine wa Afrika katika nchi ya Cameruni ambapo anaenda kuongoza Chuo cha Umoja wa Afrika Pan Afrikanism ambapo makao yake yako Yaunde Cammeruni hivyo atakuwa huko.
Pia katika hatua nyingine alifurahishwa na zawadi walizompatia kutoka Mkoa wa katavi akazielezea kuwa ni moja ya zawadi ambazo ni bora kati ya zawadi alizopewa, nkatika maeneo mbalimbali aliyopita kuagwa na wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria kwenye matawi yake yote.
Prof. Mbwete akizungumzi fursa zilzopo kwanza alishukuru kumaliza muda wake bila kusikia mgomo wa aina yeyote na hajawahi kusikia wanafunzi wala mwanafunzi yeyote katika kpindi cha miaka kumi aliyoongoza wakigoma hata kama wana matatizo ni watu wenye kuvumilia na wako tofauti na vyuo vingine.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu Huria tawi la Mkoa wa Katavi ameleza kuwa eneo lililopatikana amesaidia kuweza kununua ambapo jumla ya shilingi milioni 45 zimemika ameitoa mwenyewe kwa ajili ya kusaidia kuweza kulipa fidia eneo lile ambalo yalikuwa mashamba ya watu, akasisitiza eneo hilo lipimwe na kupatiwa hati ili ujenzi uanze.
Akaeleza kuwa iwapo litamilikiwa na Chuo litaweza kutumika kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa ya chuo, nyumba za walimu, pamoja, makitaba ya kisasa na kumbi nzuri za mikutano ambazo wanafunzi watakuwa wanafanyia semina na makongamano, pia wananchi wakihitaji watakuwa wanakodishiwa na kukiingizia chuo mapato.
Pia Chuo kimeanzisha College za Mikoa na Vituo Wilayani ili kusaidia kuwapatia eleimu wananchi walio wengi, kwa upande wa Mkoa wa Katavi ni moja ya mikoa inayofanya vizuri hususani katika darasa la TEHAMA Kwani kila mwaka wanafunzi wanaongezeka kwa kasi tofauti na Mikoa mingine.
Kuhusu Vituo vya Mikoa ya Katavi na Katavi ameeleza kuwa mikoa hiyo inaingizwa kwenye mkongo wa Taifa, iwapo mikoa hii ikingia katika mkongo wa Taifa wanachuo watanufaika sana kwa kujisomea na kpatiwa materiali kupitia kwa njia ya matndao.
Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho katika risala yao iliyosomwa na Rais wa wanachuo Yachitu ilieleza kuwa Makamu wa Chuo Prof Mbwete ni mfano wa kuigwa kwa jinsi alivyo mbunifu kiongozi hodari, mchapakazi na anayependa kusikiliza na kuendelea kujifunza na anayependa kupokea ushauri kuondoka kwake ni pengo ambalo litachukua muda kuliziba.