Mbinu Kuu za Kuepuka Matapeli wa Nyumba
*Lamudi Tanzania, yawaasa Watanzania kuwa makini kabla na baada ya kununua nyumba.
Kutokana na ongezeko la watu binafsi na mashirika yanayojenga nyumba za biashara kuongezeka kwa kasi, watanzania wamekuwa wakikadiriwa na ongezeko la utapeli wa nyumba na viwanja visiyohalali. Lamudi Tanzania, inarahisisha kupunguza utapeli katika soko hili kwa kuainisha njia kuu tatu za kuzingatia kabla ya kununua au kupanga mali isisyohamishika. Njia hizo kuu tatu ni pamoja na
1. Hakikisha nyumba au kiwanja ina Hati miliki.
hati ya nyumba au ya kiwanja ni lazima iwe inatambulika na wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya kazi, Lamudi Tanzania inashauri kwa wateja wote hata wenye lengo la kupanga wahakikishe wanaona hati miliki ya mtu anayempangisha ili kuepuka utapeli wa kupangishwa na mtu asiyehusika.
”kumekuwa na kesi nyingi ambapo wateja wengi wanakuja na lengo la kupanga lakini wanaishia kutoa pesa kwa matapeli au wamiliki wasio halali wakati mwenye nyumba hatambui kitu, hivyo ni vyema kuhakikisha anayekupangisha au kukuuzia nyumba halali awe na hati miliki inayo tambulkika na serikali”. Godlove Nyagawa –meneja mkazi wa Lamudi Tanzania alifafanua.
2. Mwanasheria na shahidi.
Kuna baadhi ya wateja wanasahau umuhimu wa mwanasheria na kuona suala la kupanga na nunua ni jambo la mazoea. Mwanasheria anasaidia hasa kama mali iliyopo sokoni si halali hivyo inakuwa si rahisi mtu kukuuzia akiwa na lengo la utapeli, si hivyo tu bali wanasheria wanasaidia kuelewa mkataba vyema iwapo utahitaji ufafanuzi wowote kuhusiana na mkataba.
Shahidi ni mtu muhimu pia ambaye anasimama kama mtetezi iwapo utatokea utapeli wowote, “ni vyema kuzingatia uwepo wa mwanasheria na shahidi bila ya kujali upande mmoja, ili kuwa na usalama iwapo atahitajika shahidi mahakani baada ya kuonekana kuna matafaruku au mgororo wa aina yoyote katika makubaliano yenu,” Godlove alifafanua
3.Hakikisha unatambua historia ya sehemu unayotaka kuishi au kununua.
Wateja wengi huwa wanasahau kufatilia historia ya sehemu anayotaka kupanga au kununua, wengi wetu huwa tunatazama bei na ubora wa nyumba au kiwanja anachohitaji , lakini kihistoria viwanja vyengine huwa na migogo ya kifamilia au serikali na jamii, “ katika miaka ya nyuma, kumekuwa na migogoro ya ardhi kama maeneo ya wafugaji na wakulima-Arusha, mabwepande-Dar es Salaam na sehemu nyingine nyingi tofauti hapa Tanzania , ambapo kuna baadhi ya maeneo mpaka serikali iweze kusimamia kati, hivyo ni vyema kutambua historia ya maeneo tofauti na kuweza kukabiliana nalo mapema kabla ya kununua” Masserat Alakhia –Afisa masoko na mahusiano ya jamii wa Lamudi Zambia,Tanzania na zimbambwe aliafafanua.
Kwa upande mwingine , Afisa masoko na mahusiano ya Jamii wa Lamudi Tanzania Lilian Kisasa Alifafanua kwamba, kuzingatia hati miliki na mikataba ni muhimu kabla ya kununua nyumba, lakini kwa upande mwingine watanzania wasijishau katika kutafuta bima za nyumba, hivyo hata mtu akishanunua nyumba ahakikishe amejiunga na bima yoyote ya nyumba ili hata ikitokea maafa yoyote aweze kurudishiwa mali zake katika kiwango chochote “Kutokana na kuwapo na majanga yasiyotabirika, Tanzania ilitengeneza sheria ya Kuratibu Misaada ya Maafa Nambari 9 ya Mwaka 1990, kwa kuboresha vifungu kadhaa vya sheria , na kuhusisha wadau mbali mbali na kutoa Muongozo wa Kukabiliana na Majanga ya kitaifa uliokua chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Pamoja na kuwepo kwa sheria hii kuwapa misaada wahanga mbali mbali , lakini bado inatupasa sisi wenyewe tujikwamue kimawazo na kujiunga na bima za nyumba ambazo zitaweza kupunguza mzigo kwa serikali, na kukupunguzia gharama zozote iwapo itatokea janga lolot”.
KUHUSULAMUDI
Ilizinduliwa 2013, Lamudi ni ya kimataifa inayolenga masoko ya juu ya mali zisizohamishika yanayoibukia kwa haraka- Lamudi inaongezeka kwa sasa inapatikana katika nchi 28 katika Asia, Mashariki ya Kati, Afrika na Amerika ya Kusini, na pia ina idadi ya mali zisizohamishika takribani 600,000 kupitia mtandao wake wa kimataifa . Lamudi ni moja kati ya kampuni zinazoongoza na bora , kutokana na kutoa huduma kwa wauzaji, wanunuzi, wamiliki wa ardhi na wakulima ambapo tovuti hii imekuwa ni salama na rahisi kutumia kupata makazi kupitia online .
kuhusuAIH
Afrika Internet Holding kampuni hii inatanguliza na kuchochea kasi ya mabadiliko ya online katika Afrika – kwa ajili ya watu wake na utamaduni wake. Pia inadhumuni la la kuleta mafanikio na umahiri katika makampuni ya internet ambayo yanaongeza mageuzi ya utamaduni wa Kiafrika wa matumizi ya internet . AIH ni kundi mama lenye makampuni tisa yenye mafanikio na yanayokua haraka katika nchi zaidi ya 25 za Afrika, na zaidi ya wafanyakazi 3000. AIH inajali kuhusu ujasiriamali na hufanikisha mambo muhimu yote yanayohitajika kuimarisha kampuni: timu, dhana, teknolojia na mitaji. Ambapo Mtandao wake wa makampuni ni pamoja na JUMIA, Kaymu, Hellofood, Lamudi, Carmudi, Zando, Jovago, Lendico na Easy taxi.
Tembelea Lamudi kupitia Facebook, Twitter, Google+ na LinkedIn