Na Kibada Ernest, Katavi
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 2.6 katika sekta tofauti. Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2014/2015 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah alieleza kuwa baadhi ya miradi ilitekelezwa katika mwaka wa fedha uliopita hususani miradi ya maji na ile ya ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi katika shule za Sekondari.
Chang’ah alisema miradi ya maendeleo ina thamani ya shs 2,968,146,617.00 bilioni imetekelezwa katika sekta ya Elimu ya Msingi, sekta ya elimu ya Sekondari, sekta ya utawala, sekta ya Maendeleo ya Jamii, sekta ya Afya, sekta ya Maji, sekta ya Barabara na sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo alieleza kuwa Sekta ya Maji miradi iliyotekelezwa iko katika vijiji vya Igagala, Ngomalusambo, Majalila, Igalula na katika eneo la gereza la Kalilankulu yenye thamani ya shilingi 1.2 bilioni imetekelezwa katika vijiji hivyo.
Sekta ya Elimu ya Sekondari, hususani ujenzi wa maboma 17 ya maabara za masomo ya sayansi yenye thamani ya shilingi 630 milioni umekamilika katika sekondari za Karema, Ikola, Ilandamilumba, Kabungu, Mwese na Mpandandogo.
Miradi mingine ni ujenzi wa nyumba ya mwalimu, ujenzi wa matundu ya vyoo 13, madarasa manne na mfumo wa maji yenye thamani ya gharama ya shilingi 160.2 milioni.
Sekta ya elimu ya msingi miradi yenye thamani ya shilingi 50 milioni imetekelezwa ikiwa katika hatua ya mbalimbali ya utekelezaji miradi hiyo ni ujenzi wa madarasa manne, matundu 13 ya vyoo, nyumba moja ya mwalimu pamoja na ukarabati wa nyumba ya mwalimu.
Sekta ya mifugo na Uvuvi miradi yenye thamani ya shilingi milioni 87 milioni imetekelezwa ikiwemo uundaji wa boti mbili, ujenzi wa majosho, na ujenzi wa vyoo katika minada mitano iliyopo katika Halmashauri.
Miradi mingine iliyotekelezwa katika mwaka 2014/2015 ni sekta ya barabara ambayo ni uboreshaji wa hali ya barabara kwa kufanya matengenezo ya muda maalum kilometa 14, matengenezo ya kawaida kilometa 19 ya maeneo korofi kilometa13 na ujenzi wa daraja moja katika kijiji cha Itunya miradi yote ikiwa ina thamni ya shs 755.2 milioni.
Miradi ya miradi ya maendeleo ya jamii yenye thamani ya shilingi 75.milioni iliyolenga kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kuboresha maisha yao ikiwemo na mafunzo juu ya matumizi ya Barcodes kwa wajasiriamali kwa bidhaa zao, ujenzi wa kituo cha kukusanyia mazao ya nyuki na ununuzi wa mashine tisa za kufyatulia tofali kwa ajili ya vikundi vya vijana.
Kuimarisha utoaji wa huduma ya afya kwa jamii, ujenzi wa nyumba ya mganga, zahanati ya Kibo, na ukarabati wa zahanati ya Kapalamsenga miradi yote ikiwa na thamani ya shilingi 25 milioni. Miradi ya sekta ya utawala imegharimu kiasi cha silingi 14.4 milioni, ukarabati wa nyumba ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kabungu, ukamilishaji wa kituo cha Polisi Tarafa ya Karema na ofisi ya kijiji Igalula.
Akizungumzia Mpango na makadilio na mwelekeo wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 18.6 Bilioni kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato.
Mkurugenzi Chang’ah alieleza kuwa jumla ya shilingi 18,646,959,311.5 kutoka katoa vyanzo mbalimbali vya mapato, ambapo matumizi ya kawaida shilingi 1.658,747,753 Bilioni,(OC) na (PE) ni 9,155,262,028 bilioni,Vyanzo vya mapato ya ndani( OS) shilingi 1,969,503,873.50 bilioni Ruzuku ya maendeleo shilingi 4,678,372,740 biloni na vyanzo vingine vya mapato shilingi 1,185,072,917 bilioni hivyo kufanya jumla ya bajeti yote kuwa shilingi 18,646,959,311.5 bilioni.
Kiasi kilichotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni shilingi 4.9 bilioni, kiasi kilichotengwa kutokana na mapato ya ndani ya halamshauri shilingi 425 milioni hivyo kufanya jumla ya fedha yote kuwa 5,412,667,740 kwa ajili ya miradi ya maendeleo itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2015/2016.
Elimu Mkoa wa Katavi umepiga hatua ya ufaulu kwa kupanda kwa asilimia kumi ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana ambapo mkoa ulikuwa na asilimia 59 kwa matokeo ya Kidato cha nne na mwaka2013 na matokeo ya mwaka 2014 mkoa umepata matokeo ya asilimia 69, hivyo kupanda kwa asilimia 10 tofauti na matokeo ya mwaka jana.
Kwa mjibu wa Taarifa ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 iliyotolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Ernest Himju ilieleza kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 yanaonesha kuwa kati ya wanafunzi 1,510 kati yao wavulana wakiwa 678 na wasichana 509 walifaulu mtihani huo kwa kupata madaraja mbalimbali.
Hinju alieleza kuwa waliopata Daraja la “Distinction”ni wanafunzi 11, Daraja la “Merit” wanafunzi 116, Daraja la “Credit” wanafunzi 283,na waliopata Daraja la “Pass” wanafunzi 619. Akaeleza kuwa waliopata daraja la Distinction ndiyo waliofanya vizuri sana,na wanafunzi waliopata Daraja la Fail ni 438 wakiwemo wavulana 280 na wasichana 158 sawa na asilimia 29.01 ya watahiniwa.
Akaongeza kuwa wanafunzi waliofanya mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2014 ni wale walioanza kidato cha kwanza mwaka 2011, wakati wa usajii ambapo jumla ya wanafunzi 1,541 kati yao wavulana 1021 na wasichana 520 wasajiliwa.
Afisa Elimu huyo alizitaja shule tano zilizofanya vizuri Mkoani kuwa ni shule ya St. Marys, PFCT Tumaini, Milala, Mwangaza, Mizengo Pinda, Kashaulili, Ikola, Katumba, Inyonga na Utende.
Akaeleza kuwa ufaulu huo ni kutokana na ushirikiano mzuri baina ya wadau wa Elimu katika Mkoa na matokeo hayo yanatoa picha ya ufaulu wa wanafunzi kidato cha nne 2014 kupanda akapongeza hatua iliyofikiwa. Akazitaka halmashauri ambazo shule zao hazikufanya vizuri kjitathmini na kubaini changamoto zilizosababisha ufaulu huo na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili zisijirudie katika mitihani mingine inayofuata.
Akizungumzia waliofanya mtihani walikuwa 1,510 wakiwamo wavulana 1,001 na Wasichana 509. Idadi hii ni sawa na asilimia 98 ya wanafunzi waliosajiliwa. Mkoa wa Katavi unazo jumla ya shule za Sekondari 37, miongoni mwa hizo shule 31 ni shule za serikali na sita ni shule binafisi, mwaka 2014 jumla ya shule 34 miongoni mwa shule 37 zilikuwa na wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha Nne. Mtihani wa kidto cha nne mwaka 2014 ulifanyika nchini kote kuanzia Novemba 03 hadi Novemba 28 2014.