ZOEZI LA UANDIKISHAJI NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY KUENDELEA ZANZIBAR NA PEMBA VIWANJA VYA AMANI NA GOMBANI

ZOEZI LA UANDIKISHAJI NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY KUENDELEA ZANZIBAR NA PEMBA VIWANJA VYA AMANI NA GOMBANI
ZOEZI LA UANDIKISHAJI NA MAJARIBIO KWA WACHEZAJI WATAKAOJIUNGA NA KITUO CHA MICHEZO CHA NSSF-REAL MADRID SPORTS ACADEMY LITAENDELEA MJINI ZANZIBAR NA PEMBA TAREHE 14/03/2015 NA 15/03/2015 KATIKA VIWANJA VYA AMANI NA GOMBANI.

1. Walengwa ni Watoto waliozaliwa kuanzia tarehe 01-01-2001 hadi 31-12-2003
2. Wawe na cheti halisi cha kuzaliwa na nakala yake.
3. Picha mbili za pasipoti zenye rangi ya bluu nyuma.
4. Watoto waambatane na wazazi wao (Baba au Mama mzazi) au Mlezi wa kisheria yaani anayetambuliwa kwa hati za kisheria.
5. Awe na vifaa vya michezo na maji ya kunywa.
6. Usajili utaanza Jumamosi saa moja asubuhi na kumalizika saa kumi jioni
7. Unguja zoezi litakuwa Amaani Stadium.
8. Pemba zoezi litakuwa Gombani Stadium.
9. Majaribio yatafanyika siku ya Jumapili kuanzia saa moja katika viwanja vya Gombani na Amani (unguja na Pemba).
10. Zoezi hilo ni bure wazazi hawatozwi chochote zaidi ya kuwanunulia vifaa na maji watoto wao.