Soko la Rangi Kushuhudia Mabadiliko Kutokana na Maendeleo ya Miundombinu Nchini

Soko la Rangi Kushuhudia Mabadiliko Kutokana na Maendeleo ya Miundombinu Nchini
KUTOKANA na mpango mkakati wa serikali wa mwaka 2012 mpaka 2017 ambao unalenga upanuzi wa makazi katika mikoa mbalimbali, kumekuwa na ongezeko kubwa la majengo ya makazi, majengo ya ofisi na majengo ya masoko ambayo yameonekana kuwa na manufaa na mchango mkubwa katika sekta mbalimbali na viwanda nchini Tanzania.

Mpango huu wa upanuzi umejenga mahitaji kwa vifaa vya ujenzi ambapo kwa upande mwingine imeonekana kuwa ni faida kwa wauzaji ambapo wauzaji wengi wamekuwa na jitihada katika kuongeza kasi na namna ya uendeshaji na utoaji wao wa huduma ili kukabiliana na mahitaji mapya.

Kama ilivyo kwa saruji na vyuma, rangi pia imekuwa ni bidhaa kubwa na moja ambayo imekuwa ikihitajika sana kutokana na maendeleo ya miundombinu. Maendeleo haya ya kasi yamesababisha mabadiliko kwenye sekta ya rangi pia ili kukabiliana na mahitaji yanayojitokeza. Hii imesababisha kuanzishwa kwa teknolojia mpya, bidhaa na njia za kibunifu ili kukidhi mahitaji muhimu kwa ajili ya ubora unaoitajika.

Katika ulimwengu huu wa teknolojia soko la rangi pia limekuwa likibadilika kuendana na maendeleo yaliyopo. Kumekuwapo na utumiaji wa mashine zinazotumia kompyuta ambazo zimepunguza muda ufanyaji kazi na kuwa msaada mkubwa sana wasanifu na makandarasi wakiwa katika ujenzi.

Haya yameelezwa na Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd. Moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Anasema kuwa “iwe kwa ajili ya nyumba, biashara au viwanda soko la rangi nchini lipo katika hatua kubwa kutokana na maendeleo ambayo yanatokea hivi sasa. Sekta hii inaweza kusimama kutokana na mchango mkubwa inayoleta katika uchumi wa nchi”

Kampuni ya Insignia ni mfano wa kampuni ndogo ambayo imepitia mitihani mingi na hatimaye imekuwa kiongozi na kuleta mabadiliko katika soko la rangi nchini. Tangu kuanzishwa kwake mkoani Moshi (Kilimanjaro) kampuni hii sasa imeonyesha matunda yake.

Bw Kishan pia ametoa maoni kwamba makampuni ya kisasa ya rangi kama vile Insignia hayana budi kudumisha ujasiriamali wake ambao umekuwa kama uti wa mgongo wa ukuaji wake. Na katika maendeleo hayo vilevile anatoa wito wa kuwa na “nia ya dhati na ubunifu ambao utasaidia katika ukuaji zaidi wa soko hilo.”

Kuanzia kwenye majengo ya makazi na majengo ya viwanda rangi inahitajika sana katika ujenzi wake. Miongoni mwa huduma mbalimbali zinazotolewa na Insignia ni pamoja na ‘THE ART’, inayotumika kulingana na mahitaji ya mteja.
Maendeleo ya makampuni kama vile Insignia kutoka biashara ndogo na kuwa kampuni kubwa ni ushahidi tosha katika soko la rangi kama moja ya sekta inayoshirikiana na sekta nyingine katika kuchagiza uso wa miundombinu ya nchi yetu.
Kuhusu Insignia
Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.
Hivi leo, Insignia imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini Tanzania umewezeshwa na ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco ya Ufaransa.
Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi. Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatengenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoedana na thamani- ya -fedha.
Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora wake. Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa.
Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.