Ofisa mwakilishi wa Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Profesa Tolly Mbwette akizungumza katika hafla maalumu ya uzinduzi wa awamu ya nne ya programu hiyo jana Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam akifundisha kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa programu maalumu ya mafunzo ya kuandaa na kuboresha mitaala ya elimu Afrika wakiwa katika kozi hiyo iliyozinduliwa leo Dar es Salaam.
Meza kuu katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.
Baadhi ya maofisa toka meza kuu wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala ikifuatilia mada anuai.
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) wamewezesha kozi kwa baadhi ya nchi za Afrika yenye lengo la kuboresha mitaala ya elimu.
Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu, Anne Kilango Malecela katika hafla ya uzinduzi wa programu hiyo ya uboreshaji mitaala, aliipongeza UNESCO pamoja na taasisi zingine zilizounganisha nguvu kuhakikisha kozi hiyo ya uboreshaji mitaala inafanyika.
Alisema njia pekee ya kuendelea kuboresha elimu yetu ni kutumia wataalamu wa elimu hasa wanaohitimu katika kozi maalumu za ubunifu na uandaaji mitaala kuiboresha mitaala hiyo kwa kuzingatia mahitaji halisi taifa moja hadi lingine.
Alisema awamu ya nne ya mafunzo hayo ya uboreshaji mitaala ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na kujumuisha wanafunzi 100 kutoka nchi 23 ambazo ni pamoja na Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Zambia, Swaziland, Niger, Senegal, Cameroon, Burkina Faso, Togo, Chad, Ivory Coast, Nigeria, Hong Kong, Liberia, Sudan Kusini, Sierra Leone, Benin na wenyeji Tanzania.
Aidha Kilango katika hotuba yake ameiomba UNESCO pamoja na mashirika wafadhili wa programu hiyo kuangalia uwezekano wa kuipanua zaidi na kuboresha programu hiyo ili kuwa na manufaa zaidi jambo ambalo alisema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wowote kufaniisha jambo hilo.
Hata hivyo aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia nafasi walioipata ipasavyo pamoja na kuifanyia kazi kitaaluma mara baada ya mafunzo hayo. Alisema elimu ya utaalamu wa mitaala ni muhimu kwa taifa lolote hivyo kutumia utaalamu walioupata kuzishauri mamlaka kuboresha elimu kulingana na maitaji.
UNESCO katika hafla hiyo iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues ambaye aliwataka wanafunzi watakao pata mafunzo hayo kutumia elimu ya utaalamu ipasavyo ili kuboresha elimu.