Mchungaji Josephat Gwajima Atakiwa Kufunga Kanisa…!

Mchungaji Josephat Gwajima

Mchungaji Josephat Gwajima

KANISA lisilo rasmi la Mchungaji Josephat Gwajima lililopo katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam limeamuriwa kufungwa na kuondoka mara moja eneo hilo.

Kwa mujibu wa barua ya wamiliki wa eneo hilo, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imemtaka Mchungaji Gwajima kuondoka eneo hilo mara moja ili kupisha shughuli nyingine za wamiliki wa eneo hilo. Taarifa zinasema kuwa Kanisa hilo kwa muda mrefu lilikuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu jambo ambalo lilisababisha usumbufu na kero kubwa za kelele kwa wakazi wa maeneo hilo.

Katika barua iliosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la Nyumba la Taifa, Bw. B Masika imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo, kwani shirika hilo limeshaanza kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE ikiwa ni ujenzi wa makazi na shughuli nyingine. 

Bw Masika ametoa siku 30 tu ambazo Machi 9, 2015 Mchungaji Gwajima anatakiwa kufunga virago na kuviacha viwanja hivyo wazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Mchungaji Josephat Gwajima afunge virago.