Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
TAMASHA la Music Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 6 hadi 8 mwaka huu, Bagamoyo mkoani Pwani katika viwanja vya Mwanakalenge. Akizungumza Dar es Salaam leo Meneja wa Tamasha hilo Richard Lupia alisema lengo ni kukazia katika kurasimisha tasnia ya muziki kuwa na umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo husika la bagamoyo ambalo ni la kihistoria.
Pia Lupia alisema kuunganisha wanamuziki na kufanya sanaa ya asili ya Tanzania inapata kuonekana katika jukwaa la kimataifa. Lupia aliendelea kusema Tamasha litashirikisha vikundi zaidi ya 30 na wasanii zaidi ya 500 ndani na nje yanchi wanaopiga muziki wa dansi, Reggae, Hip Hop, Taarab, Ngoma za Asili, Bongofleva na Ghani.
“Wasanii watapata fursa ya kujifunza jinsi ya kuunadi muziki wao duniani kwa njia mbalimbali ambapo kutakua na warsa kutoka kwa wataalamu mbalimbali kutoka pande zote za dunia” alisema.
Aidha tamasha litaendeshwa mchana na usiku ambapo mchana kutakuwa na sanaa za michoro, mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha huku semina na mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua nyingine za kimaendeleo zikiendelea.
“Tushirikiane katika kuhakikisha muziki wa Tanzania unafika katika kilele cha mafanikio pia nafasi za maombi ya ushiriki kwa wasanii bado zipo” alisema.