Wakristo Zaidi Watekwa Nyara

Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka wanakoishi

Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka wanakoishi

HOFU imetanda baada ya uwepo wa taarifa kuwa raia Wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State. Taariza zaidi kutoka kwa jamii hiyo imethibitisha kwamba zaidi ya raia 200 wametekwa nyara Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa kaskazini mwa Syria.

Inasemekana wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake na wazee. Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka. Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye silaha. Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristu hawa wa Syria ndio mwanzo unaanza kujitokeza.

Wakristo kutoka Syria wameanza kutoroka wanakoishi Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristu kimetoa madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo.

Kimedokeza kuwa zaidi ya watu mia tatu hamsini wametekwa. Huku hayo yakiarifiwa waumii wengine wa kikristu wameanza kukimbia avijiji vyao wakihofia kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State.

Na bado vita vinaendelea huku waislamu hao wakikabiliana na waasi wa kikurdi pamoja na washirika wao wa kiksristu katika Mji wa Hassaka.
-BBC