Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza wananchi kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Unguja, aliyefariki ghafla wakati akiwa katika kikao cha Chama Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa Feb 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, wakiwaongoza baadhi ya viongozi wa Serikali na wananchi wakati wa kuswalia mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Unguja, aliyefariki ghafla jana wakati akiwa katika kikao cha Chama Kisiwandui mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa Feb 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi. Picha na OMR
Baadhi ya Viongozi wa juu wa Serikali, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria maziko ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, marehemu Salmin Awadh Salmin, huko Makunduchi mjini Zanzibar. Marehemu Salmin amezikwa Feb, 20, 2015 kijijini kwake Makunduchi Zanzibar. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar Feb, 2015. Picha na OMR
Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar Feb, 2015. Picha na OMR
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, akiweka udongo katika kaburi la marehemu Salmin Awadh Salmin, wakati wa shughuli za maziko yake zilizofanyika katika kijiji cha Makunduchi mjini Zanzibar Feb, 2015. Picha na OMR