Watafutaji Nyumba Sasa Kutumia Simu, Lamudi Yarahisisa

Mkurugenzi Mtendaji wa Lamudi Tanzania, Mustafa Suleimanji (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lema (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutambulisha namba maalumu kwa wateja wenye uhitaji wa nyumba za kupanga, kununua na kuuza bidhaa mbalimbali ambao wataunganishwa.

WATAFUTAJI nyumba za kupanga, nyumba za kununua pamoja na uuzaji wa bidhaa mbalimbali nchini Tanzania sasa wamerahisishiwa kupata huduma hizo kwa kutumia simu ya mkononi.

Kampuni ya Lamudi Tanzania leo imetangaza namba maalumu ambayo itatumiwa na Watanzania ambao awali walikuwa wakihaha kuzunguka huu na kule kutafuta nyumba ama za kupanga au za kununua kwa matumizi mbalimbali.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Lamudi Tanzania, Mustafa Suleimanji alisema alisema miaka mitano iliyopita asilimia 90 ya wakazi wa jiji walikua wakizunguka kutafuta nyumba za kupanga ama kununua jambo ambalo kwa sasa linabadilika.

Alisema kwa sasa inakadiriwa kuwa Watanzania milioni 8 wanamiliki simu za mkononi mkononi hivyo ujio wa wa staili mpya ya kutambulisha namba ya simu na Lamudi ili wateja waweze kuitumia kipindi wanahitaji huduma za kutafuta nyumba za kupanga, kununua, uuzaji na ununuzi wa bidhaa mbalimbali utaleta hauweni kwa huduma hizo.

Alisema muhitaji atatakiwa kupiga namba 0800710022 na kuunganishwa na dalali na pia mmiliki wa nyumba na kuanza kufanya makubaliano papo hapo, jambo ambalo litarahisisha mambo kwa kiasi kikubwa.