IFM Yakanusha Kumpigia ‘Kampeni’ Lowassa

Edward Lowassa

Edward Lowassa


SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM-SO) YAKANUSHA KUMPIGIA DEBE LOWASSA

SERIKALI ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFMSO), kupitia msemaji wake mkuu ambaye ni Rais wa Serikali ya wanafunzi, ndugu Clinton Boniface inakanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la NIPASHE toleo namba 0578395 la tarehe 19/02/2015, lenye kichwa cha habari “WANAFUNZI WA IFM WAMTAKA LOWASA URAIS” na kwamba habari hizo hazijatolewa na uongozi wa IFMSO, wala hakuna mkutano wowote uliofanyika katika eneo la chuo cha usimamizi wa fedha kati ya waandishi wa habari na uongozi wa serikali ya wanafunzi na kutoa tamko hilo.
Pia, kulingana na Katiba ya IFMSO kifungu namba 3, ibara ndogo ya 1, Katiba inakataza serikali ya wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika mambo yoyote ya kidini au kisiasa, hivyo basi IFMSO inasikitishwa na taarifa hizo na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hizo.