Umeshasikia Kuhusu SmartPhones, SmartBelt Sasa Kuna SmartBeds

Hivi majuzi niliongelea kuhusu Smart Belt, mkanda ambao unajiongeza na kujipunguza wenyewe kutokana na jinsi ulivyoshiba. Leo nakufamisha kuhusu Luna; Luna ni “bed cover” ambayo inafanya kitanda chochote kuwa smartbed. Luna inaweza kufanya yafuatayo:
1) Kufanya kitanda upande mmoja kiwe na joto na upande mwingine kiwe na baridi
Wakati unaanza kuitumia Luna, utakuwa unaseti mwenyewe “temprature” lakini baada ya muda kidogo itakuwa imeshakusoma na itakuwa inajiseti yenyewe.
2) Luna ina kengele ambayo inakuamsha wakati muafaka, inaanza kukuamsha kwa kuongeza mwanga taratibu.

3) Inafunga milango ikiona umeshalala

4) Inazima TV au kupunguza sauti, ikiona umeshalala

ce59d1c7df2984f0bbd2f09da0347378333a3ced_feature1

Angalia video hapa chini