Valentine’s Day na Skylight Band Thai Village Masaki

Valentine's Day na Skylight Band Thai Village Masaki

Valentine’s Day na Skylight Band Thai Village Masaki

DSC_0002

Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 (wa pili kulia) akiongoza vijana wake kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kushoto ni mwimbaji Baby, Ashura Kitenge pamoja na Sam Mapenzi.

Ijumaa hii Skylight Band hawatopiga Thai Village watakua njiani wakitokea nchini Oman, wanaomba radhi kwa usumubufu wowote utakaojitokeza kwa wateja wao.

Ila siku ya Jumamosi siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Skylight Band wataporomosha burudani ya nguvu na ya aina yake kwa mashabiki wao ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku mashabiki wakipata fursa ya kuchagua nyimbo wazipendazo zinazoendana na siku hiyo maalum pamoja na kugawa zawadi kwa “couples” itakayonoga na kutokelezea.

DSC_0011

I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)…I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,…..(Aiyayaaaaa)…Mmm Take Me,….Nitembee Nawe,…..Baby Take Me, Nitembee Nawe….Aneth Kushaba AK47 akipiga kolabo na Sam Mapenzi.

DSC_0029

Kikosi kazi cha Skylight Band wakisakata lisebene.

DSC_0035

Moja ya zawadi ndani ya usiku maalum wa Valentine’s ni hii Membership card aliyoshika mdau Francis Machibya, ambayo inakupa nafasi ya kuhudhuria show zote za Skylight Band zinazofanyika Thai Village bure kwa mwaka mzima.

DSC_0134

Mashabiki wa Skylight Band wakicheza moja ya style inayofahamika kama “Yachuma chuma”.

DSC_0177

Sehemu ya umati wa mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka.

DSC_0168

DSC_0042

Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti na Aneth Kushaba AK47 pamoja na Baby.

DSC_0023

Wadau wakinywa na ku-enjoy muziki mzuri wa Skylight Band.

DSC_0069

Sam Mapenzi akikonga nyoyo za mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti na John Music pamoja na Sony Masamba….Usikikose Jumamosi hii Valentine’s day Thai Village watakinukisha.

DSC_0147

Sam Mapenzi akiongoza mashabiki wa Skylight Band kwa style ya aina yake.

DSC_0149

DSC_0151

Sony Masamba akijimwaga na shabiki wake kwenye dancing floor.

DSC_0295

DSC_0171

Katika kupika mziki mzuri wa Skylight Band ukanoga basi huyu jamaa James Kibosho, anahusika sana na hivi sasa ametua Skylight Band.

DSC_0175

Kiungo kingine chenye vipaji lukuki si mwingine ni Danny Kinanda akifanya yake.

DSC_0083

Burudani ikiendelea.

DSC_0191

DSC_0194

Pale mzuka wa mashabiki unapopanda.

DSC_0205