Boko Haramu Wasababisha Uchaguzi Kuahirishwa

Mkuu wa Uchaguzi Nigeria,  Attahiru Jega.

Mkuu wa Uchaguzi Nigeria, Attahiru Jega.

MKUU wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, Attahiru Jega, amesema upigaji kura hauwezi kufanyika nchini humo Jumamosi ijayo kwa sababu wanajeshi wanaotakiwa kulinda vituo vya kupigia kura wanatumika kupambana na kundi la Boko Haram.

“Hatari ya kutumia vijana wetu katika jeshi na kuwataka watu watumie haki yao ya kidemokrasi, katika hali ambapo hawawezi kuhakikishiwa usalama wao, ndio jukumu letu kubwa.

Wakati huo huo, Chama Kikuu cha Upinzani cha Nigeria kimesema kuwa kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu kumerejesha nyuma demokrasi. Katika hali hiyo tunaamini kuwa mashirika machache ya uchaguzi popote pale duniani yatafikiria kusonga mbele na uchaguzi kama ilivyopangwa, katika hali kama hii.”

Jega alikanusha kuwa alishinikizwa aakhirishe uchaguzi; lakini siku ya Alkhamisi tu alikuwa akisisitiza kuwa uchaguzi utafanywa kama ulivyopangwa.

Chama cha upinzani cha APC kimesema jeshi limetaka uchaguzi uakhirishwe ili kusaidia kampeni ya Rais Goodluck Jonathan. Waandishi wa habari wanasema haikuelekea kuwa usalama ndani ya nchi utatengenea sana katika wiki sita tu zijazo.
-BBC