Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali mstaafu Issa Machibya (katikati) akifungua mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio itakayofanyika kuanzia Septemba 4 mwaka huu nchini kote. Wakufunzi hao wanatarajiwa kusambazwa sehemu mbalimbali ili kutoa mafunzo kwa watu watakaoshiriki kuendesha Sensa ya majaribio. Wengine ni – Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu , Dk. Albina Chuwa (kulia) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Hafidhi (kushoto).
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa (katikati) akitoa neon la utangulizi kabla ya kukmaribisha Mkuu wa Morogoro, Kanali mstaafu Issa Machibya(kushoto) kufungua mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio yalioanza leo mjini Morogoro ambayo yamewashirikisha wadau mbalimbali. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu.
Baadhi ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio ambayo inatarajia kufanyika kuanza Septemba 4 mwaka huu wakiwa katika mafunzo ya wiki moja leo mjini Morogogoro. Wakufunzi hao wanatarajiwa kusambazwa katika maeneo mbalimbali nchini tayari nao kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa watu watakaohusika na sensa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali mstaafu Issa Machibya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa Sensa ya majaribio ambao wanashiriki mafunzo ya wiki moja ya wakufunzi wa Sensa ya majaribio itakayofanyika kuanzia Septemba 4 mwaka huu nchini kote. Wakufunzi hao wanatarajiwa kusambazwa sehemu mbalimbali ili kutoa mafunzo kwa watu watakaoshiriki kuendesha Sensa ya majaribio. (Picha zote na Tiganya Vincent, MAELEZO- Morogoro.