CCM Yapata Pigo Kubwa Njombe…!

 Aliyekuwa MNEC  wa  wilaya ya  Ludewa  Elizabeth Haule  wa  pili kushoto enzi za uhai  wake  akiwa na viongozi  wa  wilaya  hiyo wakati wa mkutano mkuu wa wilaya ya  Ludewa mwaka jana, kulia  ni mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe, aliyesimama ni mwenyekiti  wa CCM wilaya  ya Ludewa Stanley Kolimba na wa kwanza  kushoto katibu  wa CCM wilaya ya  Ludewa Eliud Semauye.

Aliyekuwa MNEC wa wilaya ya Ludewa Elizabeth Haule wa pili kushoto enzi za uhai wake akiwa na viongozi wa wilaya hiyo wakati wa mkutano mkuu wa wilaya ya Ludewa mwaka jana, kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe, aliyesimama ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba na wa kwanza kushoto katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Eliud Semauye.

CHAMA  cha  Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya  Ludewa  mkoani  Njombe  kimepata  pigo  kubwa kufuatia  kifo  cha  aliyekuwa  Mjumbe  wa  Halmashauri  Kuu ya Wilaya  hiyo (NEC)  Bi. Elizabeth Haule.

Mbali ya  kuwa MNEC  wa  wilaya  hiyo  Haule  pia  alikuwa ni mwenyekiti  wa UVCCM wilaya ya  Ludewa  kabla ya  kujiuzulu kwake mwezi  February mwaka jana baada ya  kuchaguliwa nafasi hiyo ya  NEC na  nafasi   hiyo  kuwa  wazi  hadi sasa.

Katibu   mwenezi  wa  CCM  wilaya  ya  Ludewa  Felix Haule  alisema  kuwa  kifo cha  kionozi  huyo  kimetokea  usiku  wa kuamkia leo akiwa katika  Hospitali ya  wilaya ya  Ludewa ambako  alilazwa jana  mchana kwa tatizo la  moyo.

Bw  Haule  alisema  kuwa siku ya  jumatatu wiki  iliyopita  marehemu  alipata   kuongoza  kikao  chake  cha mwisho cha baraza la vijana  la  wilaya ya  Ludewa  na baada ya  hapo hali  yake ya afya  ilianza  kuzidi  kuwa mbaya  zaidi kabla ya kuamua jana  kwenda Hospitali ambako  walimlaza.

Alisema  kuwa mazishi ya  mjumbe  huyo wa NEC  Wilaya ya  Ludewa yanataraji  kufanyika  kesho  kutwa jumamosi kijijini kwake Mholo kata ya Luana wilayani  Ludewa.

Marehemu Elizabeth Haule  enzi  za uhai  wake 

Kwa  upande wake Mbunge wa Jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe  akielezea kifo cha  MNEC  huyo alisema  kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya  kifo  hicho na kuwa kwa sasa  anafanya maandalizi ya  kuelekea  jimboni  Ludewa  ili  kuungana na  wana CCM na wananchi  wa wilaya  hiyo katika mazishi ya kiongozi huyo.

Mbunge Filikunjombe alisema  kuwa  CCM wilaya ya  Ludewa  imempoteza  kiongozi mchapa kazi na aliyekuwa na uwezo  mkubwa katika  kukitumikia  chama ngazi ya  wilaya na Taifa na  kuwa kati ya  vijana  ambao wamekuwa mbele  kujenga  chama katika  wilaya   hiyo ni pamoja na marehemu huyo kwani  siku  zote za  uhai  wake alikuwa  ni mhumini mzuri  wa kunadi  sera  za CCM na hakuwa kiongozi mwenye majivuno  wala makundi.

Hivyo  alisema  kuwa  kifo  cha MNEC  huyo kimekuja  huku  wilaya ya  Ludewa ikiwa katika maandalizi ya  kuanzimisha miaka 38  ya kuzaliwa kwa  CCM sherehe  iliyopangwa  kufanyika siku ya jumapili  ya February 8 mwaka  huu kwa mara ya kwanza katika kata ya Kilondo mwambao mwa ziwa nyasa  lakini kutokana na msiba  huo  mkubwa sherehe   hizo  zitasogezwa  mbele  hadi Februari  15 mwaka  huu.

“…Mimi pia nilikuwa  nikijiandaa  kwa ajili ya  kuanza  safari ya  kuelekea wilayani Ludewa  katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa  kwa CCM kama mgeni  rasmi ila sitaweza kufanya  hivyo na  chama  kimeamua  kusogeza  sherehe  hizo hadi jumapili ya ijayo  ili  kupisha maombolezo kwa wana CCM kwa kifo cha kiongozi huyo,”