Maagizo ya Waziri Mkuu Pinda Yaendelea Kufanyiwa Kazi na Polisi!

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda

Miezi kadhaa iliyopita waziri Mkuu Pinda alitoa maagizo wakati anazungumza bungeni kwamba Watanzania wataokuwa wanaandamana “wapigwe tu”. Tokea agizo hilo litolewe na mkuu huyu, polisi wetu wameendelea kuwa wakatili na wanyama dhidi ya Watanzania wenzao kwa kisingizio kwamba wanavunja sheria. Mimi sio hakimu, na wala sitaki kuingia kwenye mjadala kwamba wamevunja sheria au lah! Tatizo ninalo liona hapa ni uvunjaji mkubwa wa haki za binaadam kwa polisi kutumia nguvu kupita kiasiiiii. Kama tutaendelea kuchekea na kukaa kimnya dhidi ya unyama huu, basi tufahamu kwamba nyani ataendelea

kula mahindi na siku ya siku, Tanzania tutabaki na mabua. Embu angalia Video hapo chini, halafu tumia akili zako za kawaida tu (weka ushabiki wa kisiasa pembeni), halafu unambie je kulikuwa na ulazima wowote kwa polisi hawa kutumia nguvu kiasi hiki na kudhalilisha hawa wananchi wenzetu/wenzao?? Watu wanapigwa virungu kama ng’ombe (hata ng’ombe hastahili kupigwa hivyo!). Katika video hii, Polisi wanaonekana kabisa kwamba wamesheheni silaha za kila aina, sasa wanashindwa vipi kuwaweka watu chini ya ulinzi (kama wamevunja sheria) bila kuwapiga kiasi hiki? Huu umekuwa ni utamaduni wa polisi wetu wa Tanzania kwa miaka mingi sasa (kama walivyo polisi wa nchi nyingine zinazoendeshwa kibeberu), na unatakiwa ukomeshwe mara moja. TheHabari tunalaani ukatili huu, katili zilizopita, na katili zozote zijazo huko mbele ya safari….!