Na MatukiodaimaBlog
VYUNGU
vya asili vinavyotengenezwa kijiji cha Rungemba katika wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa vinaweza kusaidia kuitangaza wilaya ya
Mufindi kiutalii zaidi iwapo serikali ya wilaya hiyo
itawawezesha na kuwahamasisha zaidi wananchi wilayani humo
kujiajili wenyewe katika ufinyanzi.
Kijiji
hicho cha Rungemba ambacho kwa sasa wananchi wake hasa wanawake
wameendelea kujipatia kipato zaidi kutokana na ufinyanzi wa vyungu
na mapambo mbali mbali yatokanayo na ufinyanzi ,kimeendelea kujipatia
wageni zaidi wa ndani na nje ambao wamekuwa wakifika kupata
huduma ya kazi itokanayo na ufinyanzi.
Akizungumza
na mtandao www.matukiodaima.co.tz mmoja kati ya wanawake
wanaojishughulisha na ufinyanzi wa vyungu eneo hilo Bi Anna Kalinga
alisema kuwa awali walianzisha eneo hilo kama utani utani ila
kwa sasa eneo hilo limeendelea kupata umaarufu mkubwa na hata
gharama za vyungu na mapambo mengine imeendelea kukua zaidi.
Hata
hivyo alisema kuwa idadi ya wananchi kupenda kutengeneza vitu
vya utalii kwa kutumia udongo imeendelea kuongezeka huku baadhi ya
watu wameanza kuboresha maisha yao kwa kujenga nyumba za kisasa na
kusomesha watoto kupitia kazi za ubunifu wa kitalii.
Alisema
katika eneo hilo wanatengeneza vitu mbali mbali za kitalii
vikiwemo vitu mfano wa viatu vya kupandia maua ambavyo gharama
yake ni kati ya 160,000 hadi 320,000 kwa viatu viwili kwa maana ya
pea moja huku vyungu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 45,000
hadi 75,000 na kuwa bei hiyo imepandishwa kutokana na ongezeko la
watalii katika eneo hilo .
”
Eneo hili kwa sasa limeendelea kuwa maarufu sana kwa kutangaza
utalii na utamaduni wa kitanzania kupitia ufinyanzi ila bado
serikali haijatambua na kuelekeza nguvu zake zaidi eneo hilo kwa
kuweka utaratibu mzuri wa kuvutia watalii kufika hapa”
Mkuu
wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu akizungumzia utalii wa eneo
hilo alisema wilaya yake ilianza mchakato wa kubainisha vivutio
vya utalii pamoja na kukusudia kushirikiana na familia ya Chifu
Mwinyigumba ili kuweka mazingira mazuri eneo la makaburi kama sehemu
ya historia pindi watalii wanapofika kutembelea eneo hilo.
Wakati
kwa upande wa wasanii hao wanaotangaza wilaya kupitia ufinyanzi
za vitu mbali mbali za utalii alisema ofisi yake ilianza mwaka 2007
kwa kuwapeleka baadhi ya wana kikundi Kyela mkoani Mbeya
kujifunza namna ya utengenezaji wa vyungu bora na dhana nyingine
ili kuvutia watali zaidi japo kwa sasa wilaya hiyo haina afisa
utalii baada ya aliyekuwepo kufariki dunia mwaka jana .
Afisa
utalii kanda ya kusini Tanapa Bi Risala Kabongo alisema kuwa eneo
hilo la Rungemba ni moja kati ya maeneo ya vivutio vya utalii katika
mikoa ya kusini na kuwa wilaya ya Mufindi pamoja na vivutio
vingine bado wanapaswa kuboresha eneo hilo ili kulitumia kama
sehemu ya utalii na kuwa suala la utalii linajumhisha mambo mbali
mbali yakiwemo ya hoteli ,biashara na wanyama ,maji ,tamaduni ,na
mambo mengine mengi ambayo wageni hupenda kujifunza . |