Wafanyabiashara Iringa Mjini Wagoma

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa Iringa Mjini, kuashiria kugoma.

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa Iringa Mjini, kuashiria kugoma.

Askari  wa FFU  wakizunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa jana
kama  njia ya  kulinda amani kwa  wafanyabiashara  ambao  waliendelea
kutoa huduma  baada ya wenzao  kuwa katika mgomo
MOja  kati  ya  maduka  mjini Iringa yakiendelea  kutoa  huduma  mbali
ya  wafanyabiashara  wengine  kuwepo katika mgomo  kushinikiza
kuachiwa  huru kwa mwenyekiti wa  wafanyabiashara  Taifa  Bw  Johnson
Minja
 
Mmoja kati ya  wafanyabiashara  wadogo (machinga) mjini Iringa akiwa
amepanga  bidhaa zake  nje ya  duka moja wao  eneo la Miyomboni
kufuatilia wafanyabiashara  wenye maduka  kufunga maduka yao
kushinikiza  jeshi la  polisi  kumwachia mwenyekiti  wao Taifa ,hapa
ni  kufa kufaana
Wananchi mbalimbali  wa mji  wa Iringa  wakiwa katika  soko  kuu la
mjini Iringa  kupata  huduma  zao wakati sehemu mbali mbali huduma
zikiwa  zimesitishwa  kufuatia mgomo  wa wafanyabiashara  nchini
BAADHI ya  wafanyabiashara   mkoani  Iringa  jana  wamegoma  kuungana na
wafanyabiashara  wenzao nchini  kushiriki mgomo  wa  kushinikiza jeshi la  polisi  kumwachia  huru mwenyekiti  wao  wa chama  cha wafanyabiashara  nchini Bw.  Johnson  Minja anayedaiwa  kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
 
Wafanyabiashara  hao  waliosusia  mgomo  huo  walifikia uamuzi huo  kama  hatua ya
kupinga uamuzi  wa  wenzao ambao walifunga maduka  yao kwa  siku nzima
kuungana na  wafanyabiashara  wa  mkoa  wa Dar es Salaam  ambao walifanya  hivyo .
 
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu katika  mitaa mbali mbali  ya  mji wa Iringa na maeneo ya  nje ya  mji  wa Iringa ulionyesha  kuwa mgomo  huo  kukosa ushirikiano  kutokana na baadhi ya maduka ya  pembezoni mwa  mji  wa Iringa na yale ya  vijijini na baadhi ya maduka ya  katikati ya mji wa Iringa  kuendelea na huduma kama  kawaida huku  wakiomba  ulinzi kwa jeshi la  polisi  ili  wao kuendelea  kutoa  huduma kama  kawaida.
 
Huku cha kushangaza  hata  baadhi ya  salun na  bucha  za nyama katika baadhi ya maeneo mjini hapa  zilifungwa  huku baadhi ya maduka yanazozunguka  soko  kuu la Iringa  pia yakifungwa japo katika soko hilo umati mkubwa wa  wananchi  waliendelea kupata  huduma kama kawaida .
 
 
Mmoja kati ya  wafanyabiashara wa mji  wa Iringa Bw JOhn  sanga  alisema kuwa ameshindwa  kuungana na  wafanyabiashara  wa mji  wa Iringa katika mgomo  huo  kutokana na  shinikizo  kubwa ambalo  lilikuwa  likionyeshwa na watu  waliokuwa  wakisambaza  jumbe  za mgomo   huo  juzi na jana kupitia  kikundi  cha  watu kama 11  ambao   wengi  wao  walikuwa wakitoa  vitisho  wakati wa  kusambaza  taarifa   hizo.
 
” Kweli  nimeshindwa  kufunga duka  langu leo kutokana na vitisho  vya watu hao ambao   wanatulazimisha  kufunga kwa nguvu huku  wakitambua kuwa  si kila mfanyabiashara  ni mwanachama  wa chama  chao   hicho cha  Wafanyabiashara…kutulazimisha  kufunga  biashara  zetu ni kutunyanyasa  sisi tusio  wanachama na  tambua kila mmoja ana  maisha yake  wao badala ya  kukutana  viongozi kwa ajili ya  kulimaliza  suala  hilo  wanataka  wote  tufunge  maduka  huu ni ushauri  mbaya  kuliko “
 
Hata hivyo  alisema  hajaweza  kufunga  na ataendelea  kutoa huduma  wakati  wote wa mgomo  wa  wafanyabiashara  hao kwani  si  lazima  kila mfanyabiashara  kuungana nao katika  chama  chao na kiongozi  wao.
 
Huku mfanyabiashara  Geofrey   kalinga  akieleza  kusikitishwa na serikali kushindwa  kuchukua hatua kali kwa  kikundi hicho  cha wafanyabiashara   wachache ambao  wanachochea  mgomo huo na kuwakosesha wengine amani ya  kufungua  biashara  zao na  kuwa  kuendelea kuchelewa  kuchukua hatua  ni kubariki migomo kama hiyo  kuendelea.
 
Kwani alisema  ni jambo la  kushangaza  kuona  watu hao  wachache wakitumia nguvu  kuwazuia  wengine  kuungana nao katika mgomo  huo huku wakitambua  kuwa  chama  hicho ni chama cha hiari  kujiunga ama kutojiunga  hivyo  walipaswa  kushughulika na  wanachama  wao na sio wafanyabiashara wote.
 
“Haya ni mambo ya ajabu sana hivi  inawezekana  vipi hiki  kikundi  cha  wachache  kutulazimisha  wafanyabiashara  wote  kujiunga na chama  chao…sasa  leo  wanatutaka  kufunga  biashara  kwa  muda  usiojulikana kesho  watakuja na  jambo   jingine lakini  swali la msingi hapa  hicho chama  chao kinatusaidia nini  sisi ambao  si  wanachama tunapofungiwa  biashara zetu ya mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) kwa  kuchelewa
kulipa  kodi….ama  wanatusaidia   vipi na kodi  kubwa ya mapango ya vyumba  vya  biashara ambazo tumekuwa  tukilipa…kama  jibu  hakuna basi  watuache na  wao  waendelee na migomo yao”
 
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  wafanyabiashara   waliofunga maduka  yao walisema  kuwa  sababu ya  kufunga maduka  kwa muda  usiofahamika ni  kutoka  jeshi la  polisi  kumwachia huru kiongozi  wao kitaifa  Bw Minja anayedaiwa  kukamatwa  toka  juzi na  jeshi  la polisi na hajulikani alipo.
 
Akizungumza kwa niaba ya wananchi  wa  mkoa wa Iringa Suzana Ndelwa  alisema  kuwa  kufungwa kwa  maduka katika  mji  wa Iringa  kumewaathiri wananchi
kiuchumi kutokana na baadhi yao  kutoka  nje ya  mji  wa Iringa kufuata
huduma  za  jumla ila kufungwa kwa maduka  hayo kumeyumbisha  uchimi
wao na  wa  Taifa kwa ujumla na  kuwa  ilipaswa kwa upande wa mkoa wa
Iringa mkuu wa mkoa  huo kuingilia kati  suala   hilo  .
 
Mbali ya  baadhi yao  kutoma  kufunga maduka  yao  bado ule  usemi  wa kufa
kufaana  ulionekana  kutawala katika maeneo mengi ya mji  wa Iringa
kutokana na mgomo  huo baada ya  baadhi ya  wafanyabiashara  wadogo
maarufu kama machinga  kunufaika  zaidi na mgomo  huo kwa  kupanga
bidhaa  zao  nje ya maduka  yanayofanya  biashara  kama  zao na  kupata
wateja  zaidi kupitia  mgomo  huo  huku baadhi ya  wafanyabiashara
wakionekana  kuuzia  bidhaa  zao stoo na  wengine  kufungua maduka  yao
nusu mlingoti na  kuendelea  kutoa  huduma kama kawaida.
 
Wakati wafanyabiashara  hao  wakiwa katika mgomo   huo  mjini Iringa ,Mafinga
na  baadhi ya  wachache  wa Ilula  bado  jeshi  la  polisi lilionekana
kuweka  ulinzi  wa  kutosha katika maeneo ya  wafanyabiashara  hao
huku  askari  wa  kikosi  cha  kutuliza ghasia (FFU))  wakionekana
kuzunguka  kila  kona ya  mji  wa Iringa  ili  kuthibiti vurugu  iwapo
zingejitokeza.
 
Jitihada za  kumpata  mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ama  kamanda wa
polisi  wa mkoa wa Iringa Ramadhan  Mungi  ili  kuweza  kuzungumzia
jinsi mkoa  ulivyojipanga kumaliza tatizo hilo la mgomo ama jeshi la
polisi  lilivyojipanga  kuwalinda  wafanyabiashara  ambao  waligoma
kuungana na   wenzao katika mgomo  huo hazikuzaa matunda baada ya  simu
za  viongozi hao  wawili  kuita  bila  kupokelewa.
Chanzo: www.matukiodaima.co.tz