Dk Shein atembelea vituo vya ununuzi karafuu Pemba

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Na Rajab Mkasaba, Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameendelea na ziara yake kisiwani Pemba kwa kutembelea vituo vya ununuzi wa karafuu pamoja na kambi za karafuu na kueleza azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kulirejeshea hadhi yake zao la karafuu.

Dk. Shein alikuwa akiwaeleza wananchi wakiwemo wamiliki wamiliki wa makambi kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imechukua juhudi za makusudi za kuliimarisha zao la karafuu ikiwa ni pamoja na kuongeza bei ya zao hilo kwa lengo la kulirejeshea hadhi yake zao hilo ambalo limeijengea sifa kubwa Zanzibar duniani.

Alisema kuwa jitihada za makusudi zinaendela kuchukuwa na serikali katika kuliwekea mazingira mazuri zao hilo ikiwa ni pamoja na kurekebisha Sheria ya zao hilo, kuweka mfuko wa karafuu,kuzalisha miche mingi ya mikarafuu na mambo mengineyo.

Dk. Shein aliyasema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara yake hiyo ambapo mara baada ya kutembelea kambi ya karafuu Mahuduthi, Jimbo la Mtambile aliwahutubia wananchi na kuwaeleza kuwa mabadiliko makubwa yanatarajiwa kutokea katika kuliimarisha zao hilo.

Alisema kuwa sifa ya hadhi ya karafuu za Zanzibar ni kubwa hivyo mbali na juhudi zote zinazochukuliwa pia kuna haja kutoa elimu kwa wananchi juunya zao hilo kwa lengo lamkulirejeshea hadi yake zao lakarafuu kwa kuweza kuwafaidisha wakulima pamoja na zerikali kwa jumla.

Dk. Shein alieleza kuwa serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 36 kwa ajili ya kuingia mifukoni mwa wakulima watakaouza zao hilo ambapo kwa upande wa serikali ni asilimi 20 ambazozitasaidia katika shughuli za kuimarisha miradi ya maendeleo.

Kutokana na hatua hiyo Dk. Shein alielendelea kusisitiza kuwa mbali ya kukikosesha fedha serikali kwa kuuza karafuu kwa magendo pia, uuzaji huo wa karafuu kwa magendo inaishushia hadhi yake karafuu ya Zanzibar kutokana na wanaofanya magendo kuzichakachua karafuu kwa kuchanganya na vitu vyengine pamoja na kuzitia maji.

Pia, Dk. Shein aliwataka wakulima wa zao hilo kuitunza vyema mikarafuu ikiwa ni pamoja na kuipalilia na kuijengea mazingira mazuri kwani serikali imedhamiria kuliimarisha zao hilo.

Aidha, Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao wa Mtuhaliwa kuwa serikali imo katika mikakati ya kubuni nishati mbadala na hivi sasa imo katika kutafuta uwezo kwa kutambua kuwa ukataji wa mikarafuu kwa ajili ya nishati ya kuni kutapelekea kukwatwa kwamikarafuu na kutoweza kufikialengolililokusudiwa.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliutaka uongozi wa ZSTC kukaa pamoja na wamiliki wa makambi na kuwasilikiza changamoto zinazowakabili ili waweze kushirikiana kwa pamoja na kuangalia utaratibu wa kuwasaidia.

Nao wakulima na wenye makambi ya karafuu wameeleza kufarajika kwao na ziara hiyo ya Dk. Shein kwa kuwatembelea na kuwasiliza changamoto zao zinazowakabili na kusisitiza azma yao ya kuendelea kuuza karafuu zao kwa serikali.

Walieleza kilio chao kikubwa kuwa ni kupata mikopo kutoka serikali kwa lengo la kuendeshea shuguli zao uchumaji wa karafuu na kuahidi kufuata masharti yote yatakayowekwa na serikali hatua ambayo Dk. Shein aliutaka uongozi wa ZSTC kukaa pamoja na wakulima hao kwani nia ni kutengenezxa na kuliimarisha zao hilo.

Uongozi wa ZSTC ulipokea agizo hilo la Mhe. Rais ambapo pia ilieleza hatua kubwa iliyofikiwa katika uendelezaji wa zao hilo ikiwa ni pamoja na wananchi walio wengi kujitokeza kuuza karafuu serikalini.

Uongozi huo ulieleza kuwa licha ya kuwa ndio mwanzo wa msimu wa zao hilolakini mafanikio makubwa na matarajio yameanza kujitokeza kwa kuweza kununua karafuu kwa wingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma iliyopita.

Aidha, uongozi huo ulieleza kuwa kwa upande wa vifaa juhudi zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha vinapatikana yakiwemo majamvi, pishi na vifaa vyenginevyo ambapo tayari hapo jana zaidi ya pichi 450 za kupimia karafuu zilifika kupitia bandari ya Mkoani.

Pamoja na hayo uongozi huo ulieleza kuwa zaidi ya tani 170 zimeshanunuliwa ambapo kiasi cha shilingi Bilini 2.3 zimeshatumika kununulia karafuu.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Khafani Othman, alieleza kuwa matayarisho yote ya karafuu kisiwani huko kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi zinafanywa katika kituo hicho cha Mkoani na baada ya hapo hupekekwa moja kwa moja Unguja kwa kutiwa kwenye makontena na kusafirishwa bila ya kutoka nje ya bandari ya Zanzibar.

Katika ziara hiyo Dk. Shein alitembelea kituo cha ununuzi wa karafuu Chake Chake, Mkanyageni, kambi za karafuu zilizopo Changaweni pamoja na kutembelea kituo cha ununuzi wa karafuu mkoani pamoja na kutembelea jingo la Ikulu ndogo mkoani.

Wakati wa jioni hapo jana Dk. Shein, aliungana na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari maalum aliyowatayarishia huko katika Ikulu ndogo Chake Chake ambapo hapo majuzi alifutari na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Ikulu ndogo ya Wete.