JESHI la Polisi limeendelea kukumbwa na majanga ya askari wake kuvamiwa na kunyang’anywa silaha nyakati za usiku wakiwa kazini. Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya tukio lililotokea mkoa wa Pwani kuvamiwa Kituo cha Polisi na majambazi kuua askari na kupora silaha, Safari hii imetokea mkoani Tanga juzi ambapo askari wawili waliokuwa doria kwa kutumia pikipiki waliporwa silaha mbili aina ya SMG zenye no 14301230 na 14303545.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda zinasema watu wanaosadikiwa kuwa majambazi watatu waliwavamia askari hao walipokuwa wakila chakula katika moja ya mitaa ya Barabara ya 4 kwa Makoko. Taarifa zinasema moja wa majambazi hao alikuwa amevalia sare za Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walitumia kisu na kufanikiwa kupora silaha hizo.
Vyanzo vinaeleza majambazi hao walikuja na pikipiki wakiwa wabepakizana na baada ya kuwakaribia askari hao waliokuwa wanakula mmoja wa jambazi alikuwa peku na yule mwenye sare alionekana kana kwamba amemkamata mtuhumiwa hivyo alikuwa anaitaji msaada baada ya kuwakaribia askari mambo yaligeuka kila jambazi kupamba na askari wakitumia visu na kufanikiwa kuwapora silaha hizo mbili zikiwa na risasi.
Tukio hilo limetokea Januari 26, 2015 majira ya saa tano na nusu ya usiku. Askari walioshambuliwa na kuporwa silaha ni namba G 369 PC Mansour na H 507 PC Mwalimu wakiwa doria ya kutumia pikipiki. Polisi Tanga inamsikilia mtuhumiwa mmoja jina Ayubu Haule, umri 27, Mngoni Fundi Radio Mkazi wa Corner Amboni Kiomoni ambaye alikamatwa eneo la tukio akijaribu kutoroka na Pikipiki na mara baada ya kupekuliwa alikutwa na mchoro wa ramani unaoonyesha matokeo ya barabara. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.