Kesi ya Mubarak yaendelea nchini Misri

Aliyekuwa Rais wa Misri, Hosni Mubarak

ALIYEKUWA Rais wa Misri, Hosni Mubarak anatarajiwa kufika mahakamani kwa awamu ya pili ya kusikilizwa kwa kesi ya kihistoria dhidi yake.

Rais huyo aliyeng’olewa madarakani ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na maafisa wengine sita wa ngazi ya juu. Watu hao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi mwezi januari mwaka huu.

Ingawa raia wa Misri wanauhakika kwamba rais huyo yuko katika hali nzuri ya afya kufunguliwa mashtaka wana wasiwasi ikiwa mawakili wa Serikali wataendesha kesi hiyo kwa kasi inayohitajika.

Mapema mwezi huu Mubarak alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa amebebwa kwenye machela. Mawakili wake wanasisitiza kuwa mteja wao ni mgonjwa sana na kuna idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo hawaamini ikiwa atafika mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.

Kwa raia wengi wa Misri Rais mubarak alikuwa sawa na mungu ambaye alitawala maisha yao kuwa muda wa miaka 30. Kwa kipindi chote hicho theluthi moja ya idadi yoye ya raia nchini humo hawajamjua kiongozi wowote ule.

Ahmed Shawky al Aqabawi mhadhiri wa somomo la sikologia katika chuo kikuu cha misri anasema watu wengi wanachuki naye na wamepania sana kuona amefungwa jela. Wakuu wa jeshi ndio wanaotawala misri tangu Rais mubarak aondelewwe madarakani.

Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni uhusiano kati ya raia na viongozi wa kijeshi umekuwa mbaya. Wengi wanaamini kuwa utaratibu watakao chukua kuendesha kesi dhidi ya Hosni mubaraka ndio utakaoamua uhusiano kati ya wakuu wa jeshi na raia utakuwa Hkatika siku za usoni.