Vanessa Mdee Asaini Mkataba Kuwa Balozi Samsung

Vanessa Mdee Asaini Mkataba Kuwa Balozi Samsung
Vanessa Mdee Asaini Mkataba Kuwa Balozi Samsung
Vanessa Mdee Asaini Mkataba Kuwa Balozi Samsung
Vanessa Mdee Asaini Mkataba Kuwa Balozi Samsung
KAMPUNI ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza imehusisha kampuni hiyo na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania. Leo hii, Kampuni namba moja duniani inayoongoza kwa technolojia ya hali ya juu, Samsung wanayo furaha kumtangaza balozi wao mpya mwanamziki nyota, na mtangazaji wa Televisheni na radio Vanessa Mdee.

Katika mkutano na wanahabari ulilofanyika hoteli, ya Hyatt Regency, iliyoko mjini Dar es Salaam iliohusisha kusaini kwa mkataba baina ya Vannesa Mdee na uongozi wa kampuni ya Samsung ni ishara tosha ya makubaliano rasmi kati ya Kampuni ya Samsung na msanii huyo. Kitendo hicho kilihashiria mwanzo wa kazi mpya kwa Vanessa Mdee kama mwakilishi wa kampuni ya Samsung nchini Tanzania.

Akiwa kama balozi wa kampuni ya Samsung, Vanessa atakuwa kiungo muhimu katika muonekano na uzinduzi wa bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo. Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kielektroniki ya Samsung, Mike Seo alisema kuwa, “kwa kutambua ongezeko la uhitaji wa simu za kisasa kwa soko la kati nchini Tanzania ni bora kuwasiliana na wateja wetu kupitia mtu ambaye amebeba sifa zinazoendana na vifaa vyetu na soko letu.

Anaongeza kuwa “Tunafuraha sana kutangaza ushirikiano wetu na Vanessa Mdee akiwa kama Balozi wetu mpya nchini Tanzania. Akiwa kama mwanamziki nyota na mchangiaji chanya kwa wananchi wa Tanzania. Vanessa anawakilishi vijana wa kisasa wa Tanzania na ni mtu ambaye kampuni ya Samsung inaweza kufanya naye kazi hivyo basi tunafuraha kubwa kuwa na mtu kama huyu kuwakilisha bidhaa zetu.

“Vanessa Mdee ambaye aliongozana na menejimenti yake kwenye mkutano huo, alielezea juu ya furaha yake kwa kuwa sehemu ya kampuni ya Samsung, alisema “Samsung ni kampuni kubwa na yenye hadhi ya juu, ni heshima kubwa sana kwangu kuwa balozi wa kampuni hii inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya kielektroniki ulimwengu, huu ni mwanzo tu wa jinsi mwaka 2015 utakavokuwa wa mafanikio kati yangu na kampuni ya Samsung. Binafsi, natumaini juu ya kazi hii na nasubiri kwa hamu siku nitakayoanza kazi rasmi. “