Upimaji wa Ramani za Viwanja Katika Soko la Mali Zisizohamishika

Baadhi ya wafanyakazi wa Lamudi Tanzania.

Baadhi ya wafanyakazi wa Lamudi Tanzania.

 

UTAYARISHAJI na upimaji wa ramani  wa viwanja ni jukumu la serikali pamoja na wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya  makazi hapa Tanzania, ramani hizi ni muhimu katika matumzi tofauti hasa katika kutoa taarifa mbali mbali iwapo kutakuwa na mahitaji ya ujenzi au  matumizi ya geodetic hasa katika sekta za ujenzi na miundombinu.

Kulingana na juhudi za wizara ya ardhi katika mwaka wa bajeti 2014-2015, iliweza  kununua mashine ya gharama kwa lengo la kuchapisha ramani nzuri na zenye viwango zitakazo husiana na survey na  geodetic . Hata hivyo Wizara ya ardhi iliweka lengo la kuchapisha ramani za kutosha hasa katika jiji la Dar es Salaam, ambapo ilifikia lengo la uwiano wa 1:2,500 kwa jiji la Dar peke yake, hivyo katika mwaka 2015, serikali inaendelea kuweka lengo la kutoa ramani za kutosha na zenye viwango katika nchi nzima.

Meneja Mkazi wa Lamudi Tanzania, Godlove Nyagawa, alifafanua kwamba, kumekuwa na jitihada nyingi katika wizara husika ili kuhimiza watu waweze kupimisha viwanja vyao, lakini kuna baadhi ya wamiliki kutoka maeneo mbalimbali  ya mikoa hasa pwani na mambo ya ndani  wanaendelea kuuza viwanja vyao bila ya sheria na wengine hawana hati ya umiliki.

Aliongeza kuwa, tatizo hilo katika sekta husika si viwanja visivyopimwa peke yake, lakini pia vipo viwanja vilivyopimwa kiholela ambavyo bado vinaleta migogoro kati ya jamii na serikali au jamii na jamii. Godlove aliongezea kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini wanapohitaji kununua viwanja au nyumba na kuhakikisha kuwa ramani hiyo inajulikana wizarani.
Timu ya Lamudi pamoja na wizara husika  inapendekeza juu ya sheria ya  kupima maeneo  ili kuepuka migogoro ya adhi kama iliyotokea mabwepande,morogoro,na maeneo ya wakulima na wafugaji.