Polisi Korogwe Wakamata Milipuko na Mirungi Kwenye Basi la Abiria

Milipuko hiyo baada ya kukamatwa kwenye basi la abiria.

Milipuko hiyo baada ya kukamatwa kwenye basi la abiria.

Magunia ya mirungi yakipaiwa kwenye gari la Polisi baada ya kukamatwa kwenye basi la abiria.

Magunia ya mirungi yakipaiwa kwenye gari la Polisi baada ya kukamatwa kwenye basi la abiria.

Milipuko hiyo baada ya kukamatwa kwenye basi la abiria.

Milipuko hiyo baada ya kukamatwa kwenye basi la abiria.

TAARIFA zilizotufikia zinabainisha kuwa Jeshi la Polisi Wilayani Korogwe, limefanikiwa kukamata shehena ya gunia 16 za dawa za kulevya aina ya mirungi pamoja na milipuko inayotumika kwa uvuvi haramu na kupasulia mawe makubwa. Taarifa zinasema mirungi ilikamatwa Ijumamosi ndani ya basi la Dar Express lenye namba za usajili T 244 BXQ kwenye kituo cha ukaguzi cha Chekeri Korogwe saa nane mchana ikisafirishwa.Shehena hiyo imepelekwa kituo cha Polisi Wilaya ya Korogwe, na mtu mmoja pamoja na Konda wa Basi hilo anashikiriwa na Polisi kwa mahojiano zaidi. Juzi pia polisi

Wakati huo huo taarifa zinasema shehena kubwa ya milipuko ya hatari inayotumika kutengenezea mabomu ya uvuvi haramu wa samaki na milipuko ya kupasulia miamba migumu imekamatwa eneo la Korogwe Siu ya Jumapili wakati Jeshi la Polisi likifanya ukaguzi ndani ya Basi la KLM EXP lenye namba T491 ARB. Milipuko hiyo ambayo imesafirishwa kwa njia ambayo sio sahihi na huenda ingeleta madhara maubwa wa abiria endapo ungelitoea mtikisio mubwa kwenye gari hilo ingeweza kulipuka na kuwadhuru abiria. Uongozi wa Polisi Mkoa wa Tanga umethibitishwa kuamata shehena hizo za bidhaa na uchunguzi bado waendelea.

 

 Basi la Dar Express likiwa limesimamishwa kwa ajili ya Ukaguzi huo.

 Ukaguzi wa Basi hilo ukiwa unaendelea

 
 
 Basi Hilo baada ya Kukamatwa.