Ofisa TAKUKURU ‘Aangushiwa’ Kipigo Chrismas…!

Ofisa huyo baada ya kipigo akipatiwa matibabu.

Ofisa huyo baada ya kipigo akipatiwa matibabu.

Mwonekano wa Ofisa huyo wa Takukuru kabla ya kipigo hicho.

Mwonekano wa Ofisa huyo wa Takukuru kabla ya kipigo hicho.


WATU ambao bado hawajajulikana wanadaiwa kumshushia kipigo kikali Ofisa mmoja wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Chunya na kumjeruhi vibaya hasa sehemu za usoni. Kwa mujibu wa chanzo chetu ofisa huyo (pichani) anadaiwa kuvamiwa na watu hao maeneo ya Sai Mbeya siku ya Siku Kuu ya Chrismas na kupigwa vibaya kabla ya kutelekezwa.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa kwa sasa ofisa huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya akipatiwa matibabu kutokana na majeruhi aliyoyapata. Hadi sasa watu waliomvamia na chanzo cha kipigo hicho hakijajulikana. Taarifa zaidi zitakujia mara baada ya vyanzo wetu kuzinyaka eneo la tukio.