Ajali Lori Yazua Moto, Wateketeza Maduka, Magari

Moto mkubwa ukiwaka eneo la ajali.

Moto mkubwa ukiwaka eneo la ajali.

Wananchi mbalimbali wakishuhudia ajali hiyo huku moshi mkubwa ukiwa umetanda eneo la tukio.

Wananchi mbalimbali wakishuhudia ajali hiyo huku moshi mkubwa ukiwa umetanda eneo la tukio.


TAARIFA zilizotufikia zinasema kuna ajali imetokea maeneo ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, ambapo Lori la mafuta limegonga nguzo ya umeme kabla ya kuzua moto mkubwa ambao umeteketeza takribani maduka saba na magari eneo hilo. Taarifa zaidi zinasema ajali hiyo imetokea maeneo ya Kivesa, karibu na duka la John Shayo ambapo Lori hilo liligonga nguzo ya umeme na kupinduka kabla ya kuzua moto mkubwa ulioleta madhara hayo. Taarifa za awali zinasema hakuna majeruhi zaidi ya mali kuteketea.