Aisha Madinda Kuzikwa Leo

Aisha Mandinda

Aisha Mandinda

ALIYEKUWA mnenguaji nyota wa muziki wa dansi toka bendi ya Twanga pepeta, Aisha Madinda aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam. Awali mazishi ya msanii huyo yalikuwa yafanyike jana lakini yaliahirishwa kutokana na familia kuwa na utata juu ya kifo cha Aisha Madinda.

Mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha Madinda yaliyokuwa yafanyike Alhamis hii yameahirishwa hadi Ijumaa ili kufanyika uchunguzi wa kifo chake chenye utata. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mwanae wa kiume, Feisal Madinda hadi kifo hicho kinatokea mama yake hakuwa mgonjwa hivyo wanamashaka na kifo chake ndio maana wameahirisha mazishi jana ili uchunguzi zaidi ufanywe.

“Kimetokea tu ghafla, ni kifo ambacho sio cha kawaida ni cha utata. Serikali nayo imeamua kufanya mambo yake imeamua kuingilia kati ili tumzike tukiwa tunafahamu nini kimemfanya mpaka afariki,” alisema Feisal akizungumza na kituo kimoja cha redio.

Hata hivyo mwanamke ambaye aliupeleka mwili wa Aisha hospitali mara baada ya kifo anashikiliwa na polisi kituo cha Oyster Bay kwa uchunguzi zaidi.