Hospitali ya Apollo Yatenganisha Mapacha Walioungana Kutoka Tanzania

Hospitali ya Apollo Yatenganisha Mapacha Walioungana Kutoka Tanzania

Hospitali ya Apollo Yatenganisha Mapacha Walioungana Kutoka Tanzania

Picture2-swahiliPicture4Picture8
WATANZANIA wameendelea kufaidika kwa huduma bora za afya kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyokonchini India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumbo ni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika Novemba 17 Novemba 2014 nchini India.

Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake. Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, halikadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.

Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbalimbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11. Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyokuwa vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivyo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.

Halikadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungo husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dk. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeonanasema, “Baadayaupasuaji, moyo wa mmoja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa manne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahalapake.”

Upasuaji huu wa mafanikio wa mapacha waliounganika kutoka nchini Tanzania sio wa kwanza kufanywa na hospitali ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha wengine wa kiume waliokuwa wameungana na kujulikana na wataalamu kama Pygopagus, Ericana & Eluidi kutoka Tanzania walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa hospitali hiyo.

Matukio amabayo yamepandisha chati kwa ujumla kama kiongozi katika sekta ya afya na mfano wakuigwa na nchin yingine ikiwemo Tanzania. Hospitali hiyo ina mahusiano mazuri na nchi ya Tanzania ikitembelewa idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Tanzania kutokana na ukosefu wa huduma muhimu na za kisasa nchini.
Mapacha walioungana hutambuliwa na kupewa majina kutokana na jinsi muungano huo unapokuwa katika viungo mbalimbali vya mwili. Ikiwa aina ya mapacha waliounganika wa Thoraco Omphalopagus ndio inayoongoza kuripotiwa kwa asilimia 28% zaidi ya aina nyingine zote zinazotambulika matukio mengi ya kitokea zaidi Kusini – Magharibi mwa bara la Asia, Africa and Brazili. Katika aina hii mapacha wanakuwa wameunganika kuanzia kifuani mpaka chini ya kifua kwenda kwenye tumbo na hutumia baadhi ya sehemu ya moyo, ini na baadhi ya sehemu viungo vya mmeng’enyo wa chakula(i).

Kulingana na hospitali ya Apollo kesi zinazo husu mapacha waliounganika huwa ni nadra mathalan moja kati ya uzao 200,000 huonekana. Lakini, asilimia 60 ya hao hufariki wakati asilimia 35 hufariki katika kipindi kifupi baada ya kuzaliwa kutokana na sababu mbalimbali(ii).

Akizungumzia upasuaji huo uliokuwa na mafanikio, Dk. Prathap C Reddy, Mwenyekiti na Muanzilishi wa Hospitali za Apollo anasema, “Nikitazama katika mwaka huu wa 2014 naona maisha ya watu tuliweza kuyagusa kwa namna njema. Mbali na maumivu wanayopata watoto yatokanayo na ugonjwa, wazazi pia hupitia mshituko na mahangaiko makubwa. Nchi nyingi za bara la Afrika zinakosa tiba muhimu na mbadala na hivyo kujikuta wanakuja nchini India kupata huduma hizo muhimu na kisasa. Inafurahisha na kuleta faraja kuwa katika siku kuu hii ya Krismasi Jimmy na Carolyn watarudi nyumbani na watoto wao wakiwa ni binadamu wawili tofauti.”

Tangu mwaka 2007, jozi na neza mapacha waliounganika katika ini na utumbo kutoka sehemu mbalimbali nchini India zimeripotiwa kutenganishwa. Aradhanana Stuthini jozi pekee ya mapacha waliwahi kutenganishwa kwa upasuaji wakiwa na mioyoiliyo katika mvungu (cavity) mmoja hali sawa na mapacha Adrianan na Abriana.

Japo moja ya mapacha wa thoracoopmhalopagus Aradhan akufariki wiki tatu baadae, Adriana and Abriana na ndio aina hiyo yamapacha walio weza kuishi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.
Baada ya miezi ya matibabu, mapacha Adriana na Abriana kutoka Dar-es-Salaam watarejea nyumbani Tanzania tarehe 18 Disemba na kufika mjini Dar es Saam asubuhi ya tarehe 19 Disemba. Katika kipindi hiki cha sikukuu itakuwa shangwe kwa wazazi Jimmy na Carolyn wanaporudi nyumbani kutoka nchini India wakiwa na watoto wao wawili waliotenganishwa.
Zaidi kuhusu hospitali za apollo
Mnamo mwaka 1983, Dk. Prathap Reddy alianzisha hospitali za Apollo, Chennai nchini India. Leo hospitali hizo zimesambaa kote nchini India na miongoni mwa kampuni inayotoa huduma bora zaidi za afya duniani. Hospitaliza Apollo zimekuwa mstari wa mbele katika kuleta mapinduzi ya sekta ya afya nchini india ikiwa na vitanda 8,488 katika hospitali zake 51 kote nchini india, Asiana Africa. Maduka ya madawa 1,586 zaidi ya kliniki 92, senta 3 za watoto na wanawake, mshirika ya elimu na idara za tafiti 15. Hospitali ina hudumia zaidi ya watu milioni 37 kutoka zaidi ya 120 duniani.
Serikali ya India ilitoa a zawadi maalumu ikiwa ni kwa ajili ya kutambua mchango unaotolewa na hospitali ya Apollo kwa jamii kama shirika la afya. Mwenyekiti wa hospitali za Apollo, Dk. Prathap Reddy alizawadiwa tuzo ya Padma Vibhushan mwaka 2010. Zaidi ya miaka 28, hospitaliza Apollo zimekuwa mstari wa mbele katika huduma mbalimbali za afya kupitia teknolojia za kisasa kabisa natafiti.