Uchaguzi Katavi Wafanyika na Changamoto

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakiwa wamepanga mstari katika moja ya Vituo vya kupigia kura kitongoji cha Mnyagala Kata ya Kabungu Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakiwa wamepanga mstari katika moja ya Vituo vya kupigia kura kitongoji cha Mnyagala Kata ya Kabungu Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi.


Wasimamizi wa Uchaguzi wakielekeza namna ya kupiga kura wapiga kura walijitokeza kupiga kra mkoani Katavi Uchaguzi wa Seriklali za Mitaa.

Wasimamizi wa Uchaguzi wakielekeza namna ya kupiga kura wapiga kura walijitokeza kupiga kra mkoani Katavi Uchaguzi wa Seriklali za Mitaa.


Mmoja wa wapiga kura ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kashaulili Halmashauri ya Mji wa Mpanda kama alivyokutwa. Na Picha zote na Kibada Kibada -Katavi.

Mmoja wa wapiga kura ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kashaulili Halmashauri ya Mji wa Mpanda kama alivyokutwa. Na Picha zote na Kibada Kibada -Katavi.

Na Kibada Kibada -Katavi

UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa Katika Mkoa wa Katavi umekamilika kwa wananchi kujitokeza kupiga kura kwa kufuata taratibu kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi wa serikali za Mitaa ingawa kulikuwa na changamoto za hapa na pale kama kuchelewa kufika kwa karatasi za kupigia kura na vituo vingine uchaguzi kuahirishwa dakika za mwisho kutokana na Mgombea kukosa Sifa ya kugombea.

Akizungumzia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsanda Kata ya Ugalla kwa kile kilichoelezwa kuwa Mgombea kukosa Sifa ya kugombea baada ya kuwa kuwa amehukumiwa kifogo cha mwaka mmoja jela siku moja kabla ya uchaguzi hivyo kukosa sifa ya kuweza kugombea na nafasi hiyo kubaki wazi hadi hapo itakapotangazwa tena na mamlaka husika ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ofisa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi Betwel Ruhega ameeleza kuwa kwa mjibu wa taratibu mgombea anapokuwa amepatikana na kosa la jinai na kuhukumiwa kifugo tena cha mwaka mmoja hivyo anakuwa amepoteza sifa za kugombea uongozi hivyo hafai kuwa kiongozi tena kwa mjibu wa taratibu.

Ruhega akaeleza kuwa aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kitogoji cha Nsanda amekosa sifa baada ya kufugwa na siku moja kabla ya uchaguzi hivyo nafasi hiyo kuwa wazi, kwa mjibu wa utaratibu inabidi kuahirisha ili kutoa nafasi kwa chama kupendekeza na kuteua jina la mgombea mwingine wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.

Hivyo uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena kwa mujibu wa Kanuni taratibu na sheria za uchaguzi. Kwa upande wake Sitanslaus Makungu toka Chadema aliongeza kuwa maeneo mengine mambo yameenda kama yalivyopangwa na wananchi wamejitokeza kwa wingi kupiga kura na hivi wanasubiria matokeo.

Na taarifa zilizopatikana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Kata ya Mpandandogo wagombea nafasi ya Uenyekiti wa Kitongoji Igagala B’ wamegongana kura hivyo inabidi uchaguzi huo urudiwe upya. Kwa Mjibu wa Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mpanda Charles Linda amesema wagombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Igagala C Kijiji cha Igalala Kata ya Mpnda Ndogo wamegona kwa kupata kura sawa hivyo inabidi uchaguzi urudiwe upya.

Linda amewataja waliolingana kura kuwa ni Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti kupitia tiketi ya CCM Isaya Daud na Stanslaus Makungu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Katika hatua nyingine wapiga kura wa kituo cha kupigia kura Mnyagala walilazimika kusubiri kuanza kupiga kura majira ya saa nane mchana baada ya kuchelewa kuwafikia karatasi za kupigia kura hivyo kurazimika kusubiri hadi zilipo fika karatasi hizo wakaanza kupiga kura.

Kwa Mjibu wa Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura Steven Msomi alieleza kuwa wananchi walijitokeza tangu asubuhi kusubilia kupiga kura na hawakuchoka na hamasi ilikuwa kubwa hasa akina mama na vjiana wengi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi na hali ya usalama ni shwari.

Katika maeneo mengine Mkoani humo uchaguzi umeendeshwa kwa amani na usalama hadi kufungwa kwa vituo vya kupigia kura kullikuwa hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa zinazohusiana na uvunjifu wa amani.