Na Kibada Kibada – Katavi
SEKTA ya Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inakabiliwa na Changamoto mbalimbali hali inayofanya sekta hiyo kutafuta mbinu na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na wingi wa mifugo uliopo kuliko ukubwa wa eneo la kufugia mifugo hiyo.
Baadhi ya Changamoto hizo ni kuwepo idadi kubwa ya mifugo katika halmashauri, Uzalishaji mdogo wa mazao ya mifugo kama nyama na maziwa na kipato kinachotokana na uwepo wa mifugo hiyo katika Halamshauri. Changamoto nyingine ni upatikanaji mdogo wa mbegu bora za mifugo hususani ng’ombe, eneo dogo la malisho ukilinganisha na Idadi ya mifugo iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Pamoja na kuwepo kwa wingi wa mifugo pia magonjwa mengi ya mifugo kama ndorobo, ndigana kati na homa ya mapafu nayo ni moja ya changamoto inayoikabili sekta ya mifugo Katika Halmashauri ya Mpanda. Halmashauri ya Mpanda ambayo ni moja ya Halmashauri katika Mkoa wa Katavi ina idadi ya Ng’ombe wapatao 87,928, mbuzi 44,348, Kondoo 8,712, Nguruwe 2,237, mbwa 7425, na kuku 141.832 hata hivyo uwepo wa mifugo hiyo bado haijatumiwa vizuri na kubadili maisha ya wakazi wa Halmashauri hiyo na mkoa kwa ujumla kiuchumi na kuinua pato lao kiuchumi.
Tafiti zinaonesha iwapoidadi ya mifugo hiyo iliyopo ikitumiwa vizuri inaweza kuleta tija na kuwaondolea umasikini wananchi katika maeneo husika. Kwa mantiki hiyo wataalam wa sekta ya mifugo wanayo kazi kubwa mbele yao kuhakikisha wanatumia elimu yao kuwabadili wafugaji waweze kufuga ufugaji wenye tija tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo ufugaji umekuwa wa kutokuwa na tija na kila kukicha imekuwa ni mivutano na migogoro kati ya wakulima na wafugaji ingawa hali hiyo bado haijatokea katika Halmashauri ya Mpanda lakini tunashuhudia maeneo mengi hapa nchini hususani Mkoani Morogoro, wilaya ya Kilosa na Kilombero, Mkoani Pwani, na Arusha na Tanga wakulima na wafugaji migogoro ya kila mara.
Uwepo wa mifugo mingi katika Halamshauri ya wilaya ya Mpanda pia kumeambatana nanUharibifu wa mazingira kutokana na wafugajinhao kuhamahama na wengine kutumia njia hiyo kwa kufyeka miti na misitu kwa shughuli za kilimo kwa kuwa wafugaji walioko katika Halmsahauri ya Mpanda hao hao ndio wakulima.
Uchunguzi uliofanyika kwa baadhi ya maeneo mbalimbali Wilayani Mpanda inaonesha maeneo mengi yanaoonekena kuathiri na Uharibifu wa mazingira na iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kwa haraka maeneo hayo yanaweza kugeka jangwa.
Baadhi ya maeneo yaliyoathirwa na uharibifu wa mazingira kutokana na mifugo ni bonde la Mto Katuma ambao ni tegemeo kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi hususani Mbuga ya Katavi ya Katavi ambayo wanyama walioko huko hutegemea kupata maji kutoka bonde la mto huo ambalo hutiririsha maji yake kupitia vijito vyake kupeleka hifadhi ya Katavi.
Mbali ya kutegemewa kwa ajili ya maji ya wanyama kama viboko na wengineo pia bonde la mto huo wa Katavi ndilo linalotegemewa kwa kilimo cha mbuga unaozalishwa kwa wingi katika maeneo ya Bonde hilo na kuwasaidia kuwaingizia pato wananchi Mkoani humo.
Kwa wastani uharibifu ni mkubwa sana kwa maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa Kata za Kabungu, Mishamo, Mwese, Karema Mpandandogo Sibwesa, Kasekese kote maeneo hayo yamejaa mifugo na uharibifu wa mazingira ni mkubwa mno ukilingansha na hali iliyopo ya mifugo.
Akizungumzia hali ya uharibifu na kuoneshwa alivyoguswa na hali hiyo na kuamua kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha uharibifu huo unafanyiwa kazi kwa kutoa elimu zaidi kwa wananchi waelewe umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kuwa na mifugo michache inayoweza kuwa na tija.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah anasema hali ya uharibifu wa Mazingira ni mkubwa mno katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo,kila eneo miti inakatwa hovyo bila kujari na hatua zisipochukuliwa ipo hatari ya kutoweka kwa misitu hiyo ambayo inaonekana kuwa ni mingi lakini ukweli ni ndio huo kutabaki kweupe wakati miti ilikuwepo kilaa kota ya Wilayah ii.
Kwa kuliona hili Mkurugenzi huyo amesema Halmashauri imeamua kuchukua hatua za kuweka mikakati kwa kushirikiana na Idara ya Maliasili kuanza kuelimsha jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na kuwapa elimu wafugaji wafuge ufugaji wenye tija. Mbali ya mikakati hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na wahisani wa Tuungane na Taasisi ya Utafiti wa wanyama aina ya Sokwe yenye Makao yake Mkoani Kigoma Janegoodle (JGI) wameanza mkakati wa kuimarisha kuvijengea uwezo vijiji ili viweze kulinda misitu kwa kutumia mpango wa matumizi bora ya ardhi, pamoja n ulinzi wa mistu inayosimamiwa na vijiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah anaeleza kuwa katika Mpango huo Halmashauri imeanza kutoa mafunzo kwa kuwapeleka Vijana wanne wanne kwa kila kijiji wamepelekwa kupata mafunzo walikwenda kuhudhuria mafunzo hayo katika chuo cha Hifadhi ya wanyama pori cha Pansiasi Mkoani Mwanza kwa kipindi cha miaka mitatu.
Chang’ah anaeleza kuwa vijana waliopata mafunzo wanatoka katika Vijiji vya Lwega, Mwese, Mpembe, Katuma, Vikonge, Isenga Bulamata na Bugwe na jumla yao wapo( 17) walianza mafunzo hayo kuanzia Augosti 16, mwaka 2011 na kuhitimu Novemba 15, mwaka 2014. Kwa ajili ya kuwajengea uwezo waweze waweze kusaidia kulinda mistu na ardhi inayoharibiwa katika halmashauri hiyo na mistu kama haikulindwa iko hatarini kutoweka na kubaki jangwa.
Akizungumzia lengo kuu la kuunda kikosi cha watu 20 katika kila kijiji ambacho kitaitwa ulinzi wa mistu yaani(Forest Gurd) ambacho kitasaidia kulinda mazingira na mistu katika vijiji. Wakiwa chuoni huko walijifunza kozi za aina mbalimbali zitakazosaidia katika suala la uhifadhi wa mistu na kulinda mazingira, baadhi ya kozi walizosoma ni matumizi ya silaha, sheria ya uhifadhi wa wanyama hima sheria, uhifadhi wa mistu na matumizi endelevu ya ardhi.
Kozi nyingine ni usomaji wa ramani, huduma ya kwanza, Ikolojia na usimamizi wa ardhi na rasilimali za mistu, Hifadhi za wanyamapori, Elimu ya uhifadhi kwa jamii, na Elimu ya Sayansi ya kuwajengea jami mahusiano, elimu ambayo itasaidia katika uhifadhi wa mistu katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Akasema mafunzo yatakayofuata yataambatana na semina za kawaida kwa hao vijana na viongozi wa vijiji ili wafahamu umuhimu wa mistu, na mafunzo hayo kwa vijana yatakua endelevu lengo ikiwa ni kufanikia vijiji 15 katika Halamshauri ili waweze kulinda mistu ambayo imeharibiwa vibaya na wavamizi wa mistu.
Uanzishwaji wa kikosi cha ulinzi wa mistu ya Halmashauri cha ulinzi wa misitu ya kijiji kitasaidia kusimamia ukataji wa mistu na uharibifu wa mazingira katika maeneo ya hifadhi za mistu ya vijiji ili waweze kuilinda wananchi wenyewe kwa kuelimishwa na askari wa kikosi cha ulinzi wa mistu wanaotoka katika maeneo ya vijiji ambao wamepatiwa mafunzo na Halmashauri kwenye chuo cha wanyapori Mkoani Mwanza.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Ardhi, na Maliasli Halamshauri ya Wilaya ya Mpanda Lucas Nyambala anaeleza kuwa pamoja na kuweka mkiakati hiyo ambayo imeanza kutekelezwa kwenye vijiji pia Idara ya ardhi inatoa elimu kwa vijiji juu ya matumizi bora ya ardhi na kupima vijiji ili kila kijiji kiwe na maeneo yake ambapo wataweza kutekeleza mipango yao ya maenedeleo kweye ardhi iliyopimwa kwa kuainisha matumizi ya ardhi yao kwa kuwa itakuwa inaonesha kila eneo shughuli yake maalum tofauti na zamani hapo hata migogoro ya aerdhi na uharibifu wa mazingira utapungua kama siyo kwisha kabisa.
Kwa kutumia mpango wa matumizi bora ya ardhi kila mtu ataheshimu makubaliano hayo kwa kuwa ardhi ya kijiji itakuwa inafahamika matumizi yake hivyo hakuna mtu atakayeumia ardhi tofauti na makubaliano yaliyowekwa na kijiji, hata miji nayo itaonesha wapi huduma za jamii ziwekwe, makazi, eneo la ufugaji, kilimo na huduma nyingine zote zitakuwazimeainishwa kwenye ramani ya ardhi ya eneo husika la kijiji.
Nyambala alieleza kuwa Kwa kuanzia mpango wa matumizi bora ya ardhi na upimaji wa maeneo ya vijiji zoezi limefanyika la matumizi bora ya ardhi na kupima maeneo ya ardhi katika vijiji vya Vikonge, Majalila, Mpandandogo. mwese, Mpembe na kutolewa hati miliki za kimila baada ya kupimwa viwanja katika kijiji cha Vikonge ambapo zoezi hilo linaendelea maendeo mengine ya Kata ya Mpandandogo, Karema, Sibwesa kazi hiyo inafaa kuigwa na maeneo mengine ili kuepusha uharibifu wa mazingira.
Naye Mkuuwa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima katika suala la uharibifu wa mazingira na ufugaji wenye Tija amekuwa akilipigia keleke kila siku akaenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa anashanga kumwona mfugaji anafuga hovyo huku watalaama waliosomeshwa na serikali wapo wanashindwa kuwa saidia wananchi kuepukana na umasikni akasisitiza watumie taaluma kuwasaidia wananchi wao hapo ndipo watakapokuwa wametumia vizuri taalama yao.