SERIKALI imesema kuna kazi kubwa katika kukabiliana na changamoto za utoaji wa msaada wa kisheria kwa watoto wanaokinzana na sheria hapa nchini.Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka mmoja ya watoto wanaokinzana na sheria, Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Maimuna Tarishi alisema hiyo ni moja kati ya changamoto zinazowakabili wakati wa utoaji wa msaada wa kisheria kwa watoto hao.Alitaja changamoto nyinmgine ni kukosekana kwa miundombinu ya kushughulikia mashauri ya watoto hao kwa kutokuwepo kwa mahakama maalumu za kutosha kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya watoto , mahabusi za watoto.Nyingine ni maafisa wa ustawi wa kutosha katika mahakama zote za wilaya na mwanzo, ambapo pia watoto wanaweza kushitakiwakutokana na sababu mbalimbali za kisheria, ufunguaji wa kesi za watoto kwenye mahakama nyingine badala ya watoto na uwepo wa watoto wengi wasio na makazi na hatimaye kujikuta wanarudia kufanya makosa.Akizungumza wakati akiwakilisha taarifa hiyo Wakili wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake, Juvenal Rwegasilaalsema kwa kipindi cha mwaka huo kituo hicho kimefanikiwa kuwahudumia kesi 115 za watoto kutoka kwenye mahakama mbalimbali ambao wametoka katika mahabusi za Segerea, keko na upanga.Alisema licha ya mafanikio hayobado wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ambazo ni ugumu wa kupatikanaji wab taarifa sahihi kwa kesi za watoto, kesi kuchukua muda mrefu na baadhi ya watioto kudanganya umri.Mbali na hilo pia lisema katika sehemu kubwa ya jamii na wazazi wa watoto wengi wao wamekuwa hawajui haki za watoto hivyo kusababisha kesi kufutwa kwa kupewa fungu la fedha.Alisema kwa sasa ni vyema elimu itolewe kuhusu haki za watoto, malezi sahihi kwa watoto. (Imeandaliwa na www.habarizajamicom)
WLAC Yazinduwa Ripoti ya Watoto Waliopo Magarezani Dar
Mtaalamu wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), Victoria Mgonela, akizungumza katika uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Grace Daffa (kulia), akizungumza na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo. Kushpoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Grace
Mkurugenzi Mtendaji wa Kikundi cha Sanaa cha Kigamboni Community Centre (KCC), Nassoro Mkwesso akizungumza jinsi watoto wanavyofanikiwa wakishirikishwa katika shughuli mbalimbali hasa michezo.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkutano ukiendelea kabla ya uzinduzi.
Wahisani wa WLAC nao walijumuika kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba naa Sheria (katikati walio kaa, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa uzinduzi huo.