Kamanda UN Asema Imepata Mafanikio Makubwa…!

Mwakilishi wa kampuni ya 4Life, Nelson Benges (mwenye tai ya damu ya mzee) akielezea virutubisho mbalimbali vinavyotumika kuimarisha kinga ya mwili wa mwanadamu kwa asilimia 437 na kuufanya mwili imara na uweze kupamba na magonjwa kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi Kulia kwa Bw. Kajugusi ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo na kushoto kwake ni Programme Officer wa Shirika la UNV, Bi. Stella Karegyesa.

DSC_0001

Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Na Mwandishi Wetu

KAMANDA wa Meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katikaukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha Operesheni Atalanta,  Peter Christian Semrau, amesema jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha njia inayotumika sana na meli kuwa salama.

Akizungumza katika mahojiano ndani ya meli hiyo ambayo imetia nanga katika bandari ya Dar es  Salaam, Kamanda Semrau alisema kwamba kwa mwaka huu hapakuwepo na tukio kubwa ambalo limetikisa eneo hilo la Pwani ya Pembe ya Afrika inayopakana na Somalia na Yemen.

Alisema kuanzia shughuli za kimataifa kukabili uharamia na ujambazi baharini kuanza mwaka 2009 kumekuwepo na  ushindi wa kimataifa kutokana na kuendelea kupungua kwa matukio katika eneo hilo ambapo awali ilikuwa ni tishio kubwa.

Alisema pamoja na kupungua kwa matukio ya kijambazi na utekaji nyara kazi ambayo inatarajiwa kufanywa mwakani ni kuhakikisha kwamba mataifa yanayopakana na bahari ya Hindi yanawezeshwa kujilinda yenyewe dhidi ya matukio ya baharini.

DSC_0004

Pichani juu na chini baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania na mabalozi mbalimbali waliojumuika kwenye hafla hiyo wakisiliza risala ya Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke (hayupo pichani).

Meli hiyo ambayo inafanya doria kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Kusini imetia nanga Dar es salaam ikitokea Madagascar ambako nako ilipata mapokezi makubwa.

Operesheni Atalanta inaendeshwa na vikosi vya Umoja wa Ulaya vikilinda eneo la bahari ambalo lina shughuli nzito kwa meli za biashara

Meli hiyo ambayo itakuwa katika operesheni hadi februari mwakani itapokewa kazi hiyo na meli nyingine ya FGS Bayern.

Naye Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke akizungumza  na waandishi wa habari akiwakaribisha katika melivita hiyo alisema kwamba amefurahishwa na mchango wa taifa lake katika kuhakikisha pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Afrika inakua salama na watu wanapata huduma zinazotakiwa.

DSC_0005

Alisema moja ya kazi kubwa ya meli hiyo ni kusindikiza meli zenye vyakula au huduma mbalimbali za kijamii kwa mataifa ambayo yanashida ili kupunguza maumivu.

Alisema pamoja na meli hiyo kutia nanga  Dar es Salaam kuonesha ushirikiano wa kutosha kati ya taifa lake na Tanzania, anatarajia mwakani mahusiano ya Tanzania na Ujerumani yatazidi kuimarika hasa katika nyanza za hifadhi na maendeleo ya jamii.

Aidha balozi huyo alisema kwamba taifa lake linaongeza fedha zaidi kwa ajili ya uanzishaji wa mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania kwa lengo la kuifanya iwe na nguvu na uwezo wa kulinda wanyama hao.

Pia alisema inafikiria namna ya kufanya na meli ya MV Liemba ambayo alisema ni moja ya vielelezo hai vilivyopo vyenye maana kubwa katika uhusiano wa Tanzania na Ujerumani.

DSC_0006

Alisema meli hiyo inafaa kufanyiwa ukarabati ili kuweza kutoa huduma kandoni mwa ziwa Tanganyika.

Aidha alisifu ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania hasa kwa kuzingatia uhuru uliopo wa vyombo vya habari na majadiliano yenye afya bungeni yenye lengo la kujenga taifa lenye nguvu.

Aidha alisema Ujerumani itaendelea kukuza uhusiano na Tanzania ambayo ni nanga ya usalama kwa mataifa ya Afrika Mashariki na ukanda wa Bahari ya Hindi kwa upande wa Afrika.

DSC_0017

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha maji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck kwenye hafla maalum ya kuwapongeza na kuwakaribisha nchini Tanzania iliyoandaliwa na ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.

DSC_0022

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maafisa wa bandari ya Dar es Salaam.

DSC_0029

Sehemu ya muonekano wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck wakati hafla ya kuupongeza msafara wa kikosi cha wanamaji wa jeshi la Ujerumani kilichoongozwa na Kamanda Peter Christian Semrau.

DSC_0030

Baadhi ya makanda wa kikosi cha wanamaji wa jeshi hilo wakilinda lango kuu la kuingia ndani ya meli hiyo.

DSC_0036

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.

DSC_0038

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh akihoji jambo kwa mmoja wa wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck ambaye jina lake halikuweza kufahamika kiurahisi.

DSC_0032

Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.

DSC_0071

DSC_0065

Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.

DSC_0057

Wageni waalikwa wakiendelea kupata picha ya kumbukumbu na Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta kubabili maharamia.

DSC_0059

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke katika picha ya pamoja na  Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi huo, John Meirikion.

DSC_0069

Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakipata picha ya pamoja ndani ya meli hiyo ya kivita.

DSC_0070

Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, John Meirikion akipata picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga bandari ya Dar es Salaam.

KAWAIDA

Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
KAMANDA wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta,  Peter Christian Semrau, amesema jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha njia inayotumika sana na meli kuwa salama.
Akizungumza katika mahojiano ndani ya meli hiyo ambayo imetia nanga katika bandari ya Dar es  Salaam, Kamanda Semrau alisema kwamba kwa mwaka huu hapakuwepo na tukio kubwa ambalo limetikisa eneo hilo la Pwani ya Pembe ya Afrika inayopakana na Somalia na Yemen.
Alisema kuanzia shughuli za kimataifa kukabili uharamia na ujambazi baharini kuanza mwaka 2009 kumekuwepo na  ushindi wa kimataifa kutokana na kuendelea kupungua kwa matukio katika eneo hilo ambapo awali ilikuwa ni tishio kubwa.
Alisema pamoja na kupungua kwa matukio ya kijambazi na utekaji nyara kazi ambayo inatarajiwa kufanywa mwakani ni kuhakikisha kwamba mataifa yanayopakana na bahari ya Hindi yanawezeshwa kujilinda yenyewe dhidi ya matukio ya baharini.

Pichani juu na chini baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania na mabalozi mbalimbali waliojumuika kwenye hafla hiyo wakisiliza risala ya Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke (hayupo pichani).
Meli hiyo ambayo inafanya doria kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Kusini imetia nanga Dar es salaam ikitokea Madagascar ambako nako ilipata mapokezi makubwa.
Operesheni Atalanta inaendeshwa na vikosi vya Umoja wa Ulaya vikilinda eneo la bahari ambalo lina shughuli nzito kwa meli za biashara
Meli hiyo ambayo itakuwa katika operesheni hadi februari mwakani itapokewa kazi hiyo na meli nyingine ya FGS Bayern.
Naye Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke akizungumza  na waandishi wa habari akiwakaribisha katika melivita hiyo alisema kwamba amefurahishwa na mchango wa taifa lake katika kuhakikisha pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Afrika inakua salama na watu wanapata huduma zinazotakiwa.

Alisema moja ya kazi kubwa ya meli hiyo ni kusindikiza meli zenye vyakula au huduma mbalimbali za kijamii kwa mataifa ambayo yanashida ili kupunguza maumivu.
Alisema pamoja na meli hiyo kutia nanga  Dar es Salaam kuonesha ushirikiano wa kutosha kati ya taifa lake na Tanzania, anatarajia mwakani mahusiano ya Tanzania na Ujerumani yatazidi kuimarika hasa katika nyanza za hifadhi na maendeleo ya jamii.
Aidha balozi huyo alisema kwamba taifa lake linaongeza fedha zaidi kwa ajili ya uanzishaji wa mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania kwa lengo la kuifanya iwe na nguvu na uwezo wa kulinda wanyama hao.
Pia alisema inafikiria namna ya kufanya na meli ya MV Liemba ambayo alisema ni moja ya vielelezo hai vilivyopo vyenye maana kubwa katika uhusiano wa Tanzania na Ujerumani.

Alisema meli hiyo inafaa kufanyiwa ukarabati ili kuweza kutoa huduma kandoni mwa ziwa Tanganyika.
Aidha alisifu ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania hasa kwa kuzingatia uhuru uliopo wa vyombo vya habari na majadiliano yenye afya bungeni yenye lengo la kujenga taifa lenye nguvu.
Aidha alisema Ujerumani itaendelea kukuza uhusiano na Tanzania ambayo ni nanga ya usalama kwa mataifa ya Afrika Mashariki na ukanda wa Bahari ya Hindi kwa upande wa Afrika.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke akifanya cheers na mmoja wa makamanda wa jeshi la wanamaji kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck inayofanya doria ya kubaini maharamia kwenye pwani ya ukanda wa Bahari ya Hindi.

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha maji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck kwenye hafla maalum ya kuwapongeza na kuwakaribisha nchini Tanzania iliyoandaliwa na ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.

Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maafisa wa bandari ya Dar es Salaam.

Sehemu ya muonekano wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck wakati hafla ya kuupongeza msafara wa kikosi cha wanamaji wa jeshi la Ujerumani kilichoongozwa na Kamanda Peter Christian Semrau.

Baadhi ya makanda wa kikosi cha wanamaji wa jeshi hilo wakilinda lango kuu la kuingia ndani ya meli hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh akihoji jambo kwa mmoja wa wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck ambaye jina lake halikuweza kufahamika kiurahisi.

Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.

Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.

Wageni waalikwa wakiendelea kupata picha ya kumbukumbu na Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta kubabili maharamia.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke katika picha ya pamoja na  Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi huo, John Meirikion.

Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakipata picha ya pamoja ndani ya meli hiyo ya kivita.

Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, John Meirikion akipata picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga bandari ya Dar es Salaam.

Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
www.mohammeddewji.com/blog
+255714940992.