Wazazi Southern Highlands Mafinga Wachangia Sekondari

Mkurugenzi  wa  shule ya  Kimataifa ya  Southern Highlands  Bi Mary  Mungai  akieleza  mipango  mikakati ya  shule   hiyo pamoja na ujio wa  shule mpya ya  sekondari.

Mkurugenzi  wa  shule ya  Kimataifa ya  Southern Highlands  Bi Mary  Mungai  akieleza  mipango  mikakati ya  shule   hiyo pamoja na ujio wa  shule mpya ya  sekondari.

Mkurugenzi  mtendaji  wa  shule   ya Southern Highlands Mafinga  Bi Mary Mungai kushoto  akiwa na  wageni mbalimbali
Wanafunzi  wa shule ya  Southern Highlands Mafinda wakipiga  vyombo  vya muziki  walipokuwa  wakiimba  wimbo wa Taifa siku ya mahafali ya  chekechea na siku ya  wazazi shuleni hapo
Mwalimu Bi  Sarah akijitambulisha mbele ya  wazazi
Wageni  mbalimbali wakiwa katika  hafla ya  siku ya  wazazi
WAZAZI wa wanafunzi  wanaosoma shule ya  Kimataifa  ya  Southern Highlands  Mafinga  wilaya ya Mufindi  mkoani  Iringa   wamechangia  kiasi cha zaidi ya Tsh  milioni  5  kwa  ajili ya  kuunga mkono  jitihada za uongozi wa  shule  hiyo kuanzisha  shule ya  sekondari  inayojulikana kwa  jina la  Mufindi Highlands School.
 
Michango hiyo ambayo  ni fedha taslimu na ahadi  ilitolewa  jana  wakati  wa mahafali ya chekechea na  siku ya  wazazi shuleni hapo kufuatia  wazazi hao  kuvutiwa na taarifa ya mkurugenzi  wa  shule  hiyo  kuhusu uanzishwaji  wa  shule  mpya ya  sekondari.
 
 
Mmoja kati ya  wazazi  hao Blankson  Ponela ambae  alijitolea  ahadi ya kuachangia kiasi cha Tsh  milioni 1.5 alisema  kuwa amevutiwa  zaidi na jitihada za  uongozi  wa  shule   hiyo kwa  kuanzisha shule ya sekondari yake.
 
Kwani  alisema  kuwa  awali  wanafunzi  wanaofaulu katika  shule   hiyo wamekuwa wakipata  wakati mgumu  kuzoea mazingira ya  shule za sekondari  ambazo wanafunzi wake wametoka katika  shule  za  msingi  za  serikali ambao  uwezo wao huwa na chini ya  ule wa  wanafunzi waliotoka katika  shule hiyo ya Southern  Hihglands ambayo  wanafunzi hujifunza  lugha mbali mbali  ikiwemo ya  Kiingereza na kifaransa na Kiswahili.
 
“Tunapenda  kuupongeza  uongozi  wa  shule  hii kwa kuja na  wazo la kuwa na  shule  ya  sekondari yake ambayo  itawachukua wanafunzi  wanaofaulu katika shule hii ya msingi …binafsi na  familia  yangu  kwa ajili ya kuunga mkono   hili ninaahidi  kuunga  mkono kwa  kuchangia  kiasi cha
Tsh  milioni 1.5 ili  kufanikisha  ujenzi huo,”
 
Huku Bw Peter Ole Mamasita alisema  kuwa  kwa  mkoa  wa Iringa shule  hiyo ya  Southern  ndio  imeendelea  kuwa  shule  yenye  rekodi nzuri ya ufaulu  wa wanafunzi ukilinganisha na  shule nyingine za binafsi na serikali.
 
 
Hivyo alisema  kuanzishwa kwa shule hiyo ni imani  kubwa  kwa wazazi katika wilaya  ya Mufindi na nje ya  wilaya   hiyo  kuendelea  kunufaika  na matunda ya  shule   hiyo  hasa kwa  kuendelea kuwafanya  watoto wao kupata  elimu  ya chekechea ,msingi  hadi  sekondari   wakiwa   katika eneo  moja badala ya  kuanza  kutafuta shule  nyingine  nje ya  wilaya hiyo.
 
Mkuu  wa  shule  hiyo Jonson Nyabuto alisema  kuwa shule  hiyo kwa  huu 2014 ilikuwa na  wanafunzi 48 na wote  walifaulu kujiuga na  sekondari na kuifanya  shule  hiyo katika matokeo  ya mtihani  huo  kitaifa kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 167  kimkoa nafasi ya nane kati ya shule 458  na kitaifa kuwa shule ya 353 kati ya  shule zaidi ya 15,867 hivyo kwa matokeo  hayo shule  hiyo imeweza kupanda kwa wastani wa pointi tano  zaidi ya mwaka jana.
 
Alisema kwa mwaka jana shule  hiyo ilifaulisha  pia  wanafunzi wote  47  na kushika nafasi ya pili   kiwilaya  nafasi ya  9 kimkoa na kitaifa  kuwa shule ya  288.

Mkurugezi  mtendaji  wa  shule   hiyo Mary  Mungai  alisema  kuwa  ujenzi wa  shule  hiyo  kwa awamu ya kwanza  unategemea  kugharimu kiasi  cha Tsh milioni 50  kwa kujenga  mabweni mawili kwa ajili ya  wavulana na
wasichana pamoja na madarasa  manne na  nyumba  moja  ya  mwalimu .


Aliwaomba   wadau mbali mbali wa ndani ya nchi na nje ya  nchi   kusaidia  ujenzi  huo wa  shule ya  sekondari kwa kuchangia  michango  yao kwa M-Pesa  0754651966 ama 0752840884 kwani  alisema upatikanaji  wa  fedha  hizi ni mgumu  zaidi  iwapo ataufanya  peke  yake  ila kama wadau  mbali mbali  wataunganisha  nguvu zao uwezekano wa kumaliza  ujenzi  huo kwa  wakati upo.

Hata  hivyo  alisema  awamu ya  pili  itakuwa  ujenzi wa maabara  ya  kiasasa, kuongeza nyumba vya madarasa, nyumba  za  walimu  na  kuwa shule hiyo  inatarajiwa  kujengwa kwa awamu  tatu hadi  kukamilika kwake  na jumla ya Tsh bilioni 1  ndizo  zinahitajika   ili kukamilisha  ujenzi
wa  shule  hiyo ya  sekondari  japo alisema mchakato  wa  kuanza
kupokea wanafunzi  kwa ajili ya  kuanza kidato cha kwanza  utaanza
mapema  mwaka  huu na mwakani  shule   hiyo  ya  Southern Highlands
Mafinda  itakuwa pia na wanafunzi  wa  kidato cha kwanza kupitia shule
yake ya  sekondari ya Mufindi Highlands School.
Mkurugenzi huyo alisema kwa wazazi wanaotaka watoto wao kujiunga na shule hiyo nafasi za masomo kuanzia chekechea , darasa la kwanza hadi la tatu wanaotokea kiswahili medium schools na la tano pia wakati, Darasa la 4 na 6  wanaotoka English medium. 


Huku  wale  wa la nne na sita wale wanaotoka English medium schools  wanaweza  kujiunga na shule  hiyo kwa kujaza fomu  za kujiunga
zinazopatikana shuleni Mafinga na kutakuwa na interviews tarehe 13 / 12/2014 maeneo yafuatayo. Shuleni Southern Highlands   Mafinga,  Oyster Bay Primary school, Dar es salaam, chuo cha Nursing Ilembula na Misufini primary school,  Songea ama  kuwasiliana na  uongozi  wa  shule kwa simu  hii 0756749151 au 0754651966 
Pia  alisema  sekondari form one wanazo  nafasi na  jina la sekondari;  Mufindi
Highlands School 

Alisema  kuwa  shule  hiyo  ni  moja kati ya  shule  bora katika wilaya ya Mufindi na mkoa  wa Iringa pamoja na Taifa na kwa kuwa toka ianzishwe  kwake haijapata  kufelisha hata  mwanafunzi  mmoja  zaidi ya  kufaulisha wanafunzi  wote  darasa la  saba .