Prof. Tibaijuka Jiuzulu Kulinda Heshima Yako na Chama

Profesa Anna Tibaijuka

Profesa Anna Tibaijuka

PROF. ANNA TIBAIJUKA BORA UJIUZULU KULINDA HESHIMA YAKO NA CHAMA

MUHESHIMIWA Bi. Anna Tibaijuka (Mb) Waziri wa Ardhi ni moja wa viongozi wachache sana wenye ujasiri na kiongozi muwazi katika sakata zima la akaunti ya Tageta Escrow, kwani kiongozi huyu amekiri wazi kuwa amepokea fedha shilingi billion 1.6 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering Bw. James Rugimalira.

Si jambo jema kumhukumu Mheshimiwa Anna Tibaijuka, lakini siyo vibaya kumshauri kwa kuwa amekuwa muwazi katika sakata hili, basi lingekuwa jambo la maana sana kama angejiuzulu madaraka aliyonayo katika serikali ili kulinda heshima yake na ya chama tawala.

Msomi yoyote yule anapofikia kuitwa Profesa na tena Waziri mwenye kushika dhamana ya nchi na wananchi yaani, Ardhi na Makazi, halafu akakubali kupokea fedha ya kiasi kikubwa hivyo bila ya kutia shaka yoyote kama ananuliwa kwa namna moja au nyingine kutokana na dhamana ya cheo chake, litakuwa ni jambo jema kwake kujiuzulu ili aonyeshe mfano bora kuwa yeye ni kiongozi mkweli na viongozi wengine wafuate nyao.

Msomi aliyefikia daraja la juu kabisa tunamwona kama kiongozi anayejua wazi kuwa yeye ni mojawapo wa Mawaziri wachache ambao Wizara zao zina dhamana kubwa ya nchi, leo hii akikubali kununuliwa kiurahisi au kufanya biashara akiwa katika madaraka mazito, tuna mashaka naye ikiwa atandelea kututumikia wananchi katika Wizara ambayo pia inahusika na mipaka ya ardhi ya nchi.

Watanzania tunajiuliza, hivi Anna Tibaijuka yupo katika utumishi wa umma tena na huku akiwa Mkurugenzi wa Mashirika.
Maoni haya yameandikwa na kutumwa hapa na: Projectus Ishengoma, Msomaji wa Mtandao huu