BAADA ya kusubiriwa miezi kadhaa, Kampuni ya kielektroniki ya Samsung Tanzania imeongeza rasmi mwanafamilia mpya katika simu aina ya Note. Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Terrace, Slipway ni alama ya uzinduzi rasmi na upatikanaji wa Samsung Galaxy Note 4 katika soko Tanzania.
Tukio hilo la uzinduzi lilijumuisha watu mashuhuri ndani ya Mkoa wa Dar es salaam ambao walipata nafasi za VIP. Watu hao ni pamoja na uongozi wa Kampuni ya Samsung, Viongozi wa Serikali, wasambazaji wa Samsung, waandishi wa habari, wadau na watu maarufu.
Kama Simu nzuri na ya kisasa ya mwaka Samsung Galaxy Note 4 inatazamiwa kuteka soko Tanzania. Simu hiyo imetengenezwa kutokana na maoni na marejesho ya watumiaji. Na pia inadhihirisha na ni ushahidi wa maendeleo na uwezo wa kiteknolojia wa akili ya kisasa. Miongoni mwa sifa zake nyingi inakuja na S pen iliyoboreshwa zaidi. Katika simu mpya ya Samsung Galaxy Note 4, S pen imeimarishwa na kufanya kuandika kuwa halisi zaidi.
Pia simu hiyo ina brush ambayo umfanya mtumiaji kuhisi kama anaandika kwenye karatasi. Air commands inayopatikana kwenye simu pia, umruhusu mtumiaji kutengeneza mahudhui kwa urahisi zaidi. Photo Note, inaruhusu mtumiaji kuchukua picha ya maandishi kutoka sehemu flani na kubadili maandishi hayo katika S Note.
Kwenye Uzinduzi wa Samsung Gallaxy Note 4, Meneja mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Mr Mike Seo, aliongelea furaha waliyonayo katika kuzindua simu hiyo. Pia Aliezelea safari yao ya utengenezaji wa simu aina ya Note iliyoanza mwaka 2011 ampapo wataalamu wa viwanda waliwashauri kuwa”Hakuna mtu atayeweza kununua simu za kisasa zenye kioo kikubwa”. Mabadiliko ya mahitaji ya watumiaji yameifanya kampuni ya Samsung kuendelea kubaki kama kiongozi kwenye utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki. Kutokana na simu za Gallaxy Note kufanya vizuri sokoni, makampuni yaliyokuwa yakiwakatisha tamaa yanafuata nyayo zao pia.
Simu hii sio tu ongezeko jingine katika familia ya Note bali pia ni mwenza wa maisha ya kisasa ya watanzania. Kampuni ya vifaa vya kielektroniki inadhihirisha uthamini na kujitoa kwao kwa wateja wao katika utengenezaji wa Gallaxy Note 4 kwani ujio wa simu hii umetokana na muunganiko wa maoni na mrejesho wa watumiaji na pia ukuaji wa technolojia umechangia katika utengenezaji wa simu hii.
Katika kumalizia kuelezea kazi ya simu hiyo, Mr. Seo anasema ”Simu ina nguvu ya kufanya hisia zako kuwa za kidigtali” Imeundwa kwa fremu nzuri ya chuma na mfumo wa kitechnolojia wa 4.4 Android (Kitkat) pia ina pen na karatasi vinavyoendana na utamaduni wetu. Ina kioo chenye upana wa 15mm.
Uzinduzi wa simu hii ulitanguliwa na kampeni ya pre oder wiki mbili zilizopita. Wateja walipata nafasi ya kuweka oda ya simu hiyo. Kampeni hiyo itawawezesha wateja 100 kujipatia zawadi ya Gia S. Gia S ni saa ya kisasa ya kampuni ya Samsung. Saa hii ina fanya kazi kipekee mbali na simu, inampa mtumiaji uwezo wa kupiga simu. Saa hii ina fanya kazi kipekee mbali na simu, inampa mtumiaji uwezo wa kupiga simu, kutuma meseji, ina blututhi na pia ina 3G Wi-Fi inayoweza kumuunganisha mtumiaji kwenye mtandao
Tukio la uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 4 halikuwa kwaajili ya kutambulisha simu hiyo katika soko la Tanzania pia ilikuwa ni sherehe ya mafanikio ya Samsung.
Waliohudhuria katika tukio hilo ni, Katibu mkuu wa mkuu wa wizara ya mawasiliano, sayansi na technolojia, Patrick J Makungu. Katibu huyo ameipongeza kampuni ya Samsung kwa kusaidia kukuza technohama nchini Tanzania. Kampuni hii imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika wizara kutokana na biashara yake sio tu kwa kukuza uchumi wa nchi bali pia imesaidia kukomesha bidhaa bandia nchini.
Professor Patrick anaongeza kuwa” Vifaa hivi vinatengeneza maisha yetu ya kila siku, tunavitumia kazini na nyumbani pia. Pia vinawakilisha jamii ya kitanzania ya kisasa kama kwingineko duniani wanavoendana na technolojia. Simu ina mchango mkubwa kwa kiwanda, chanzo kikuu cha mawasiliano kwa wafanya biashara, wawekezaji na watanzania wote kwa ujumla.
Simu hii ya kisasa inapatikana kwa Tsh 1,500,000/- inakuja na bandle ya Vodacom ya 5GB worth. Simu mpya ya kisasa ya Galaxy Note 4 itapatikana katika maeneo yafuatayo.
Maduka ya Samsung Dar es Salaam: Samsung Mlimani city, Samsung NHC House, Samora Avenue, Samsung JM Mall, Samora Avenue. Mwanza: Samsung Mwanza along barabara ya Nyerere. Arusha: Samsung Arusha barabara Themi, Barabara ya Sokoine na Agakhan. Dodoma: Samsung Dodoma barabara ya Nyerere.
Vodacom Shops
Vodashop Mlimani City, Vodashop NHC (Dsm), Vodashop Oysterbay (Dsm), Vodashop Quality Centre, Vodashop Arusha na Vodashop Mwanza. Kwa kumalizia Bw Mike Seo anatoa wito kwa watanzania kupitia kwenye duka la Samsung ya lililopo ili kujipatia hicho anachoahidi kuwa” uzoefu mzuri usiosaulika kutoka kwa Galaxy Note 4”
Kuhusu Samsung Electronics Co. Ltd
Samsung Electronics Co, Ltd ni kampuni ya kimataifa inayoongoza katika teknolojia na kufungua fursa mpya kwa watu kila mahali. Kwa njia ya uvumbuzi na ugunduzi, unabadilisha ulimwengu wa TV, simu za kisasa, Tablet, Kompyuta, kamera, vyombo vya nyumbani, Printa, mifumo ya LTE, vifaa vya tiba, semiconductors and LED solutions. Tumeajiri watu 286,000 katika nchi 80 na mauzo ya kila mwaka ni $ 216,700,000,000.
Kujua zaidi tafadhali tembelea www.samsung.com.