Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (katikati) akiongoza majadiliano kati ya wamiliki wa mitandao ya kijamii Tanzania na wataalamu wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (katikati) akiongoza majadiliano kati ya wamiliki wa mitandao ya kijamii Tanzania na wataalamu wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Assah Mwambene akifunga mkutano wa Bloggers Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Blogu Tanzania, Joachim Mushi (kulia) ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa dev.kisakuzi.com (www.thehabari.com) akizungumza kwenye mkutano wa Bloggers Tanzania.
Makamu Katibu wa Kamati ya Muda ya Bloggers, Shamim Mwasha akizungumza katika mkutano wa wamiliki wa blugu Tanzania. mitandao ya kijamii Tanzania wakiwasilisha maoni yao katika mkutano wao
Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Blogu Tanzania walioteuliwa kuongoza mchakato wa usajili wa Chama cha Wamiliki wa Blugu Tanzania wakiwa katika meza kuu.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii Tanzania wakiwasilisha maoni yao katika mkutano wao.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wamiliki wa Blogu Tanzania wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wamiliki wa Blogu Tanzania wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wamiliki wa Blogu Tanzania wakiwa katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
WAMILIKI wa Mitandao ya Kijamii Tanzania wameteua viongozi wa muda ambao watafanya kazi ya kushughulikia usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya kijamii (Bloggers) ili kuwaunganisha waendeshaji wa mitandao hiyo ya kijamii Tanzania.
Uteuzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mlimani City kwenye mkutano wa mafunzo ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) uliowakutanisha wamiliki wa mitandao hiyo ili kutoa mafunzo kwa ajili ya kuhakikisha mitandao ya kijamii inazingatia maadili kwenye kazi zao hasa kuelekea chaguzi mbalimbali zinazokuja nchini.
Walioteuliwa katika mkutano huo ni pamoja na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa dev.kisakuzi.com (www.thehabari.com), Joachim Mushi ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Bloggers na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Francis Godwin ambaye ni mmiliki wa Blogu ya Matukio Daima.
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Katibu wa Kamati hiyo, Khadija Kalili na Makamu wake Shamim Mwasha Mmiliki wa Mtandao wa 8020 Fashion Blogu. Wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo ya Muda ni pamoja na William Malecela (Lemutuz) Mmiliki wa Blogu ya Wananchi, Henry Mdimu Mmiliki wa Mdimu Blogu, Othuman Maulid mmiliki wa blogu kutoka Zanzibar, Aron Msigwa kutoka Idara ya Habari Maelezo.
Pamoja na mambo mengine kamati hiyo itashughu mchakato wa usajili wa Chama cha Wamiliki wa Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network) kwa msaada wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).