Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo kuhusu masuala
ya haki za binadamu wakifuatilia hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mhe. George Masaju (hayupo pichani) iliyotolewa leo Kunduchi
Beach Resort. Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa Taasisi za Kitaifa
za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya
mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg
(RWI) ya Sweden na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG)
kwa ufadhili wa SIDA.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akibadilishana
mawazo na Mwakilishi wa Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na
Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden, Ms. Janne Holck
Clausen (katikati) na Mratibu wa Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki
za Binadamu Afrika (NANHRI), Ms. Flavia Mwangovya muda mfupi baada ya
ufunguzi rasmi wa warsha ya mafunzo ya siku tano kwa taasisi za
kitaifa za haki za binadamu Afrika huko Kunduchi Beach Resort leo.