Waalikwa wakiwa wamejinafasi na makulaji na vinywaji.
Rehema na rafiki yake Tina wakiwa katika pozi pale lango kuu!
Ma DJ, ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja, walikuwepo kurusha roho za wadau ipasavyo!
Bi. Rehema alikuwepo lango kuu kuwapokea wageni na tabasamu zito!
Mtanzania, Rehema Edson akiwa amepozi kwenye lango kuu la kuingilia ukumbuni.
Rungwe Jr. akiwa amepiga pozi na “meya wa mji wa kairo” ndg. Ubuguvu.
Bwana harusi na Bi harusi wakipata baraka za watoto.
Watoto pia walikuwepo.
Picha na ujumbe maalum kutoka Ubalozi wa Tanzania, Misri.
mapozi na bwana na bibi harusi.
muda wa kuwapongeza bwana na bibi harusi uliwadia.
Mmoja wa waasisi wa mtandao huu, ndg. Rungwe Jr. nae alikuwepo kuiwakilisha thehabari. Pembeni yake (mwenye suti kali) ni mdau Ismail. Kama uonavyo kazi ilikuwa inaenda na dawa.
Bwana harusi na Bi harusi wakipata picha na wadau.
Wadau wakipata picha na bwana harusi (kati), Ndg. Ramadhani.
Wadau wakiendelea kuyarudi mangoma. Yaani ukumbi ulikuwa hautoshi!
Wageni wakicheza muziki.
Bibi harusi, Bi Mariam(mwenye kiremba kati) akiwa na rafiki zake Watanzania waliokuja kujuika nae.
Jana (8/11/2014) Ndg. Ramadhan Abdullahi (Mkenya) na Bi. Mariam Masalu (Mtanzania) walifanya sherehe kubwa ya harusi yao jijini Kairo, Misri tokea walipofunga ndoa miezi michache iliyopita. Sherehe hiyo inasemekana ni moja ya sherehe kubwa zilizojumuisha Watanzania, Wakenya, na wadau wa mataifa mengine kutoka Afrika. Haikuwa sherehe tu iliyohusisha bwana Mkenya na bibi Mtanzania, bali ilikuwa ni mkusanyiko wa Waafrika, ambao ulionyesha kabisa kwamba ile ndoto ya “United States of Africa” inawezekana! Thehabari inachukua nafasi hii kuwapongeza maharusi hawa, na kuwatakia kila la kheri katika ndoa yao.
Habari, picha, na maelezo kutoka kwa thebabari.com, Kairo, Misri.