Burkina Faso Kufanya Uchaguzi Mkuu Novemba 2014

Luten Kanal Isaac Zida

Luten Kanal Isaac Zida


Burkina Faso Kufanya Uchaguzi Mkuu Novemba 2014
VYAMA vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia katika nchi hiyo.
Hata hivyo mazungumzo hayo yamemalizika bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na suala la nani awe kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa raisi wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore.
Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka ya tangu aondolewe madarakani kutokana na maandamano ya raia waliokuwa wakishinikiza Rais Compaore.
Umoja wa Afrika jumatatu wiki hii imetoa muda wa wiki moja kufanyika kwa mabadiliko ya utawala na kukabidhiwa kwa wananchi na siyo jeshi tena.
Luten Kanal Isaac Zida ambaye ni kiongozi wa mpito wa kijeshi ameahidi kufuata ushauri huo wa umoja wa Afrika kwa kukabidhi madaraka kwa wananchi ndani ya muda huo wa wiki mbili.

-BBC