Washindi 100 Kuzawadiwa SamSung Gear S, Kifaa cha Galaxy Note 4

Simu za Samsung Galaxy Note 4
KAMPUNI ya vifaa vya kieletroniki ya Samsung imezindua kampeni ya kuweka oda kwabidhaa yake mpya ya Galaxy Note 4 nchini Tanzania, ikiwa ni sehemu ya kushamirisha uzinduzi mkubwa utakofuatia wa bidhaa inayosubiriwa kwa shauku ya Samsung Galaxy Note 4. Kampeni hiyo itakayoendeshwa kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi14 Novemba 2014, inadhamiria kuwapa wateja wake wakudumu nafasi ya kujipatia bidhaa hiyo ya kisasa zaidi katikafamilia ya simu za kiganjani za Note. Hali kadhalika kampeni itawawezesha wateja 100 kujipatia zawadi ya Gear S ambayo ni saa za kisasa za Samsung inayo tumika sambamba na simu hiyo.
Wakati ulimwengu wa teknolojia ya simu za kiganjaniukipanuka zaidi na zaidi, kila mwaka kampuni ya Samsunghutoa bidhaa mpya ili kuwapa wateja wake uwanja mpana wakupata kumiliki na kutumia bidhaa zenye teknolojia ya kisasa nahali ya juu kuendana na mabadiliko daima ya teknolojia.
Katikamiongo iliyopita, bara la Afrika limekuwa kama mtazamaji kwamaendeleo ya teknolojia ya simu za viganjani zilizokuwazikianzishwa kwenye soko la kimataifa. Siku hizo za utazamajizimepitwa na wakati. Enzi zile mtu kumiliki simu za teknolojia ya kisasa ilikua kwa yule aliyetoka safari ughaibuni au ndugu ametoka ughaibuni na zawadi ya vifaa hivyo, leo kampuni za simu zinatuletea vifaa hivi vya kisasa mlangoni kwetu.
Ongezeko la nguvu za nchi za kiafrika katika nyanja mbalimbali inahashiria bara la Afrika ni soko muhimu kwa nyakati hizi kulinganisha na hapo mwanzo. Ukuaji wa mara mbili zaidi ya bara la Asia, soko la simu za kiganjani la Afrika linaonyesha ukuaji wa kasi, tukio ambalo kampuni za simu ulimwengunihalijashindwa kulitambua.

Ikikatisha mfumo wa kuzindua bidhaa mpya katika masoko ya kimataifa na yaliyoendela ya barani Ulaya, Marekani, Korea ya Kusini na Asia, Kampuni ya simu za mkononi ya Samsung katika miaka ya karibuni imekuwa ikipeleka bidhaa zake kwa soko ya ndani Afika.
Gwiji la kampuni za simu za viganjani la Samsung limekuwa likizindua bidhaa zake kadha wa kadha za kisasa katika nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara, ikiwemo uzinduzi mpya wake wa simu yake mpya ya Samsung Galaxy Note 4. Uzinduzihuo, ambao awali ulifanyika huko Afrika ya Kusini, unategemea kufanyika nchini Tanzania katika siku za usoni.
Katika kusubiri shamra za uzinduzi wa simu hiyo mpya inayotarajia kufanyika Novemba 14, 2014, Samsung wanatoa nafasi za pekee kwa wateja wake wa Tanzania kuwa wa kwanza kununua na kumiliki Samsung Galaxy Note 4 kupitia oda hiyo.
Utoaji wa oda hiyo utafanywa kwa muda wa wiki mbili kuelekea kwenye uzinduzi utakaofanyika jijini Dar es Salaam. Oda hizo zitawapa pia wateja wapya nafasi kuwa katika mstari wa mbele wa kumiliki simu hiyo mashuhuri inayo subiriwa kwa shauku kubwa na wadau. Ili kuweka oda, wateja wanatakiwa kufanyamambo 3.
Hatua ya kwanza: Wajisajili kwa kujipatia Galaxy Note 4 katika tovuti www.galaxynote4.co.tz au kwa kutembelea maduka ya wakala yalioidhinishwa na Samsung na kuhakikisha wanatunza kuponi zao za oda. Hatua ya pili: Nunua bidhaa hiyoya Note 4 kutoka katika maduka husika siku ya Novemba 14, 2014 na kutunza receipt ya manunuzi. Hatua ya tatu: Baada ya manunuzi ya bidhaa husika, mteja anapaswa kujiunga na program ya E-warranty. Kujiandikisha kwa ajili oda mwisho 5:59 usiku wa tarehe 14 Nov. 2014 wakati kujiunga na E-warranty wateja wanabidi kutuma SMS ya IMEI namba ya simu zao za Note 4 kwenda 15685 mfano reg*123456789123445# kwenda 15685. IMEI namba inapatikana katika simu ilionunuliwa katika sehemu ya kuweka battery ama kwa kupiga *#06#.
Droo ya kushindania zawadi za bidhaa za Gear S za Samsung itafanyika kwa tarehe itakayotajwa baadae kwa watejawatakaokuwa wamekamilisha hatua zote tatu. Samsung itazawadia wale watakao ibuka washindi katika droo hiyo kwa Gear S bidhaa ambayo inatumika sambamba na Note 4, na ilikumuezesha kila mtu kuwa mshindi mwisho wa siku, watakaokuwa hawajabahatika kujishindia Gear S watapata kava za simuya note 4.
Gear S ni vifaa vya kisasa kutoka Samsung iliyo kwenyemuundo wa saa ambayo inaleta uzoefu wa simu mkononi mwamteja. Vifaa hivyo vyenye muundo wa saa ya mkononivinamuezesha mtu kupokea na kupiga simu, pamoja namawasiliano kutumia Bluetooth na intaneti ya 3G.
Simu mpya ya Galaxy Note 4 imetengenezwa kwa fremu ya chuma iliyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa. Simu hiyo yasaizi ndogo inakupa urahisi kuweka kwenye mfuko ikiwa nakioo kipana zaidi kutosha kuangalia muvi. Kioo chakekinauwezo wa kuonyesha picha zenye muonekano mzuri kinachosindikizwa na kalamu ya kisasa inayomwezesha mtumiaji kuandika kwa mfumo wa kidigitali. Simu hii inauwezo wa kuchaji kuanzia asilimia 0 mpaka 50% kwa dakika 30. Kama ilivyo kwa simu aina ya Galaxy S5 simu hii pia ina mfumo wa kutunza chaji ambao unaruhusu kuhifadhi chaji kwa ajili ya matumizi ya muhimu ya simu pale chaji inapoisha kabisa.

Bw. Mike Seo, Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania anasema, “Simu za mkononi zimekuwa zaulazima katika ulimwengu wa sasa, hivyo sio budi kwa makampuni ya simu za kiganjani kutambua mahitaji ya sokolake. Soko la Tanzania linaonyesha kukua kwa kasi kwa wanunuzi na watumiaji wa simu wenye hulka kadha wa kadha. Kutokana na ukweli huo, tunashauku ya kuwatengenezea wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya kisasa zaidi zitakazo wapa matokeo ya kipekee, na wateja wetu wategemee kupata hicho kutoka Samsung Galaxy Note 4 na sio kingine.”

Kutokana na ongezeko la uelewa wa wateja kuhusu umuhimu wa vifaa vya teknolojia