VYAMA vinne vya upinzani nchini, ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD vilisaini makubaliano ya kushirikiana pamoja na kusimamisha mgombea mmoja katika chaguzi zote zijazo kwa mwaka 2014. Vyama hivyo vimeibuka na nguvu mpya baada ya kuunganishwa na hoja ya kutetea Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ilielezewa kuwa ilitokana na maoni ya wananchi na hivyo kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupambana na wajumbe wa CCM kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Jumapili ya Oktoba 26, 2014 wenyeviti wa vyama hivyo, Profesa Ibrahimu Lipumba (CUF), Freeman Mbowe (Chadema), James Mbatia (NCCR- Mageuzi) na Dk Emmanuel Makaidi (NLD) walisaini makubaliano ya ushirikiano huo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Jangwani. Zifuatazo ni picha za matukio ya muungano huo.
Picha zote na Joachim Mushi wa dev.kisakuzi.com