Matukio Katika Picha UN Family Day

Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora akijumuika na timu ya Umoja wa mataifa kushangilia ushindi huo huku wakiimba.

Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora akijumuika na timu ya Umoja wa mataifa kushangilia ushindi huo huku wakiimba.

Timu ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (jezi za blue bahari) na timu ya wafanyakazi wa Wizaya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimenyana uwanjani kwenye UN Family Day iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya michezo Gymkhana ambapo timu ya Umoja wa Mataifa iliibuka kidedea kwa kuinyika timu ya Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bao 3-0.

Timu ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa (jezi za blue bahari) na timu ya wafanyakazi wa Wizaya ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimenyana uwanjani kwenye UN Family Day iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya michezo Gymkhana ambapo timu ya Umoja wa Mataifa iliibuka kidedea kwa kuinyika timu ya Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bao 3-0.

DSC_0176

Pichani juu na chini ni baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na watoto wa wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipojumuika pamoja mwishoni mwa juma kushiriki michezo mbalimbali kwenye UN Family Day kusheherekea maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanishwa kwake.

DSC_0388

DSC_0184

Watoto wakifurahia kupakwa rangi usoni katika bonanza la UN Family Day ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.

DSC_0608

Watoto wakionyesha michoro yao kwa mpiga picha kwenye bonanza la UN Family Day.

DSC_0371

DSC_0384

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakishangilia ushindi baada ya kuibuka kidedea kwenye mechi ya kirafiki na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa katika kwenye bonanza la UN Family Day lililofanyika mwishoni mwa juma.

DSC_0379

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Philippe Poinsot nao walijumuika na wafanyakazi wenzao katika UN Family Day kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar.

DSC_0412

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem (mwenye t-shirt nyeupe) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye bonanza la UN Family Day wakijiandaa na zoezi la kukabidhi medali kwa timu zilizocheza mechi ya kirafiki.

DSC_0422

Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem, Mwakilishi Mkazi wa FAO, Diana Templeman, Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakipata picha ya pamoja kabla ya kukabidhi zawadi kwa timu zilizomenyana kwenye bonanza la UN Family Day.

DSC_0440

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwavisha medali timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa iliyonyukwa bao 3-0. Kulia ni Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.

DSC_0455

Kapteni wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kukabidhiwa kikombe.

DSC_0481

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akikabidhi kikombe kwa Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza iliyoibuka kidedea kwenye mechi ya kirafiki bonanza la UN Family Day.

DSC_0482

Kapteni wa timu ya Umoja wa Mataifa Laurean Kiiza akifurahia kikombe walichokabidhiwa baada ya kuitandika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bao 3-0.

DSC_0490

DSC_0520

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) akifurahi jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Rufaro Chatora kwenye bonanza la UN Family Day ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.

DSC_0542

Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw. Titus Osundina.

DSC_0390

UN Care waliweka mabanda kwa ajili ya kutoa elimu ya afya ikiwemo ya Uzazi wa mpango, Ugonjwa Ebola, Upimaji wa VVU na ushauri nasaha, kansa ya matiti na mengine mengi kwenye bonanza la UN Family Day lililofanyika mwishoni mwa juma.

DSC_0209

Watoa huduma za afya wakifanya kipimo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliohudhuria bonanza la UN Family Day kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.

DSC_0215

Mtoa ushauri nasaha  na upimaji wa VVU kutoka Angaza (kushoto) akimsikiliza na mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kabla ya kumfanyia vipimo.

DSC_0233

Mmoja wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika banda lake la kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola

DSC_0230

Muonekano wa moja ya mabanda ya kutoa elimu ya afya katika bonanza la UN Family Day.

DSC_0221

Petra Karamagi wa ofisi za Mratibu Mkazi akibadilishana mawazo na MC wa UN Family Day, Usia Nkhoma Ledama kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar.

DSC_0163

Maakuli yalihusika pia….kazi na dawa..!