Wananchi Bukina Faso Waandamana Kumpinga Rais

Blaise Compaore

Blaise Compaore

KUMETOKEA vurugu kubwa baina ya maelfu ya waandamanaji na maofisa wa polisi katika Mji Mkuu wa Burkina Faso, Ougadougou wakati maelfu ya raia wa nchi hiyo walipokuwa wakihudhuria mkutano kupinga marekebisho ya Katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Maofisa wa usalama walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya wanadamanaji hao ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwenye majengo ya bunge. Waandamanaji hao wanapinga kubadilishwa kwa katiba ya nchi hiyo ambayo itatoa nafasi kwa Rais Compaoure kugombea tena nafasi ya urais wa nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Hata hivyo kama ilivyotarajiwa katika maandamano kama haya maofisa wa polisi kama kawaida walikabiliana na wanadamanaji hao kwa mabomu ya machozi. Hadi sasa hakuna taarifa za watu waliojerehiwa au kupoteza maisha katika vurugu hizo. Tayari vyuo vikuu, shule na maduka yalifungwa kwa wiki moja kabla maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa.

Rais Blaise Compaore alishika madaraka ya nchi hiyo baada ya kuipindua serikali tangu mwaka 1987 ambapo alichaguliwa katika kwa njia ya kidemokrasia kwa kipindi cha miaka miwili mwaka 2005. Katika mahojiano na BBC hivi karibuni Rais Blaise Compaore aliwahi kusema kuwa atafanya mambo kwa maslai ya nchi hiyo. Rais Compaire tayari ameshinda uchaguzi wa nchi kwa vipindi vinne. Hata upinzani umekuwa ukihamasisha raia kumpinga na kumlazimisha kuondoka madarakani ifikapo mwaka ujao.
-BBC