Kila Mtanzania Kupata ‘Smart Phone’ Bei Karibu na Bure

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shown some historical items as he visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on  his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shown some historical items as he visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on  his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit
to Vietnam today October 28, 2014.


KILA Mtanzania nchini atakuwa na uwezo wa kupata simu ya kisasa na yenye uwezo mkubwa (smart phone) kwa bei ya chini kabisa katika miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2020 kwa mujibu wa mipango ya kampuni mpya ya simu inayojiandaa kuingia katika soko la simu la Tanzania. Aidha, Kampuni ya Viettel ya Vietnam imemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Oktoba 27, mwaka huu, 2014 kuwa itateremsha kwa kiasi kikubwa bei ya simu za kawaida na smart phone, ili kuwezesha kila Mtanzania kuwa na simu.

Kampuni hiyo pia imemwambia Rais Kikwete kuwa itasambaza mawasiliano ya internet kwa kila kijiji nchini na kuwa kwa taasisi za umma kama vile shule, hospitali, vituo vya polisi zitapatiwa huduma hiyo bila malipo yoyote. Rais Kikwete ameambiwa habari hiyo njema kwa Watanzania na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu ya Viettel wakati alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo mjini Hanoi kwenye siku yake ya kwanza ya ziara yake rasmi ya Kiserikali katika Vietnam.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo ya umma ambayo inamilikiwa na Jeshi la Vietnam, Nguyen Manh Hung amemwambia Rais Kikwete kuwa Viettel inakusudia kumwezesha kila Mtanzania kumiliki smart phone kwa kupunguza bei ya simu hiyo na pia kupunguza bei ya huduma muhimu kama vile ile ya internet. Hung amesema kuwa Kampuni yake inapanga kupunguza bei ya simu za kawaida hadi kufikia dola za Marekani 15, sawa na shilingi 25,000 na punguza ile bei ya smart phone hadi kufikia dola za Marekani 40, sawa na shilingi 65,000. S asa hivi, bei ya simu hizo ni kubwa mara nyingi ya kisai hicho kinachokusudiwa.

“Tunataka kuifanya bei ya kununua smart phone kuwa mara 10 chini ya bei ya kununua kompyuta. Tunasukudia pia kupunguza bei ya matumizi ya simu kuwa dola moja tu ya Marekani, sawa na shilingi 1,600, kwa watu wa kawaida kwa mwezi na kwa wale ambao wanatumia simu kwa huduma nyingi zaidi watalipa dola za Merakani 50, sawa na shilingi 78,000, kwa mwezi,” amesema Hung.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a souvenir photo with workers of the Garment 10 Corporation textile mill he visited at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a souvenir photo with workers of the Garment 10 Corporation textile mill he visited at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on
his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014. PHOTO BY IKULU.


Mwenyekiti huyo amesema kuwa Kampuni yake itawekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni moja katika huduma za simu na huduma nyingine katika Tanzania na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya pili nyuma ya Peru kupata mfumo wa simu wa kisasa zaidi miongoni mwa nchi ambako Kampuni hiyo ina shughuli zake. Amesema kuwa ndani ya miaka mitatu tokea Kampuni hiyo kuanza shughuli zake katika Tanzania, kiasi cha vijiji 4,000 ambavyo kwa sasa havina mawasiliano vitapatiwa huduma hiyo katika awamu ya kwanza.

“Katika awamu ya pili, kiasi chavituo 150 vya polisi, hospitali za umma 150, ofisi za Shirika la Posta kiasi cha 65 nchini vitapatiwa huduma ya mawasiliamo yakiwemo ya internet bure katika mwaka wa kwanza wa Kampuni hiyo kuanza shughuli zake. Tutatoa pia huduma ya internet na mfumo wa teknolojia ya mawasiliano bure kwa shule 450 za umma katika wilaya 150 ambazo tayari zina umeme, huduma ambazo pia zitatolewa katika mwaka wa kwanza wa Kampuni hiyo kuanza kazi,” amesema.

Hung amesema kuwa Kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1989 iliingia katika shughuli za simu mwaka 2000 na kuanza shughuli za simu za mkononi mwaka 2004. Mwaka jana, mapato ya kampuni hiyo yalikuwa ni dola za Marekani bilioni 9.1 na kati ya hizo kampuni hiyo ilikuwa imepata faida ya karibu dola za Marekani bilioni moja. Rais Kikwete aliwasili mjini Hanoi, Oktoba 27, 2014 kuanza ziara rasmi ya siku mbili ya Kiserikali nchini Vietnam akitokea Jamhuri ya Watu wa China. Kwenye Uwanja wa Ndege wa Noi Bai mjini Hanoi, Rais Kikwete amepokelewa na viongozi wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam na baada ya mapumziko mafupi, Rais Kikwete amekwenda Kasri ya Kirais kukutana na Rais Truong Tan Sang kwa mazungumzo ya faragha na baadaye kwa mazungumzo ya Serikali kati ya Tanzania na Vietnam.

Mara baada ya kuwasili kwenye Kasri hiyo, Rais alipokelewa na Rais Sang na akakagua gwaride la heshima ambalo liliundwa na Jeshi la nchi hiyo lililokuwa na vikosi vya anga, maji na nchi kavu. Baada ya mazungumzo hayo, Marais hao wawili walishuhudia utiaji saini wa Makubaliano katika Usafiri wa Majini (Marine Transport) ambao umetiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwa niaba ya Tanzania na Waziri wa Usafirishaji wa Vietnam, Mheshimiwa Dinh Li Thang kwa niaba ya nchi yake.

Mbali na kukutana na Rais Sang, Rais Kikwete baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, Nguyen Phu Trong, ambaye pia ndiye kiongozi mkuu wa nchi hiyo. Viongozi hao wawili wamekutana kwenye Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho cha Kikomunisti, yanayoangaliana na Kasri ya Rais.